In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 91 Nakuaga matembezi, niruhusu Twaliyani Kukufariki siwezi, ila ni umaskini Nataraji matumizi, na cha kulipa wadeni Niruhusu Twaliyani, nakuaga matembezi Ni matembezi na haja, hiyo nnayobaini Nami inshallah takuja, sikukhuni abadani Japo mwezi mara moja, kama meli ya rauni Niruhusu Twaliyani, nakuaga matembezi Unapo haja thakili, mpenzi wanitamani Takuagiza mahali, hapo nendapo sakini Kwa Muhindi Ghulamali, atrafu za Chanoni Niruhusu Twaliyani, nakuaga matembezi Ukifika Kilegeza, fuliza Mkadiani Na hapo tena uliza, utadulishwa Chuleni Na mimi nitaagiza, Chonga na hadi Kungeni Niruhusu Twaliyani, nakuaga matembezi ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NAAPA USIKU SENDI Msamiati mdhana kisirani senendi sendi; siendi mahana wasiwasi hitizama nikitazama akituna akivimba; akifura mwivi mwizi swahibu zina mzinifu; mtu anayezini Sendi usiku wa giza, umenipiga mdhana Usiku ni makengeza, senendi nisipoona Makubwa sitaweleza, yamenipata mahana Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! Usiku naapa sendi, yananitosha ya jana Mengiya katika lindi, kutoka sijuwi tena Sishuki wala sipandi, hitizama rai sina Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! 92 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Nimepoteya mwituni, miti inaposongana Japo tazama sioni, marefu wala mapana Mtu usiku haoni, kujuwa fungu na kina Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! Siki usiku ni mtu, hiyo yakini si dhana Fungo hugeuka chatu, ghadhabuze akituna Kumfika huthubutu, ki-mbwa yuwadangana Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! Akhuwa mtembeyao, usiku una namna! Masiki huvaa nguo, kiwatu yakafanana Tena yana mashituo, shati muhadhari sana Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! Wendao ni maluuni, taweleza kwa majina Mchawi na shaitwani, mwivi na swahibu zina Na wao hawakutani, daima hukimbiyana Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! Kaditama namaliza, baada haya kunena Rabbi nondolee giza, na majiba kunichoma Nami nakoma susuza, kwa enziyo Subhana Sasa takwenda mchana, naapa usiku sendi! NDEGE WAMERUFUKIWA Msamiati wamerufukiwa wamepigwa marufuku mnyoo mnyororo makhunasi watu waovu Mwinyi kuondowa miko, ilani tumeletewa Ni khamsini viboko, na mnyoo atatiwa Basha uwinja hauko, tuleni vya kununuwa Ndege wamerufukiwa, wawinja tahadharini! Jamii ya makhunasi, sasa mmevunjikiwa Ambao mu majasusi, mwendao kulla kisiwa Mkawapiga risasi, mitungo mkachukuwa Ndege wamerufukiwa, wawinja tahadharini! ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ...

Share