In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

9 WAKAGWA Wakagwa walipotoka Got Ramogi walitelemka hadi Imbo Kadimo na pale walikaa muda mrefu, wakiwa na matatizo pamoja na vita kila mara na watu wa Imbo Kadimo, hata wakaamua Ndego Pindi, baba wa Obwago Ndego. Jambo hili lilichukiza Obwago na kumpa wasiwasi mwiingi mno kwamba watamalizika. Na Obwago akaanza kuwapigia wenzake kelele akisema, “Tuhame tuende ng’ambo, hapa tumechoshwa na vita kati yetu na wa Imbo, pia hapa tutamalizika, ni heri tuende Sakwa.” Wote walikubaliana, na miji ya Obwago ilitangulia na Otago, Osoro, Kan, Oboge wa Nyikidi pamoja na mtoto wake, aitwaye Obunde. Wakati huo Nyikidi baba wa Obunde alikuwa ameisha fariki. Wakagwa waliingia Sakwa na baada ya kukaa pale Sakwa tena vita kati ya Kagwa na Sakwa ilianza tena, maana kwa kweli watu wa Kagwa walikuwa ni wachokozi na tena walikuwa ni shujaa na ni wapenda vita. Lakini kwa uchache wao, ulifanya waogope na kuanza kutawanyika ovyo wakati vita ilipoanza, na koo zingine kutoroka bila kungojea vita. Hata hivyo Kagwa kweli hawakustahili kuwa wakaaji maana walikuwa 9 KAGWA The Kagwa came from Got Ramogi and moved down to Imbo Kadimo where they settled for a long time. They they began to experience troubles and frequent wars with the people of Imbo Kadimo, especially under the leadership of Ndego Pindi, the father of Obwago Ndego. This matter made Obwago made him angry, thinking that they might even be finished off in this place. So Obwago began to make noise among his community members, saying, “let us move and go to the other side, here we have had enough of these wars between ourselves and the Imbo. Here we might be finished off, it is better to go to Sakwa.” All of them agreed and the homestead of Obwago went in front of everyone, along with Otago, Osoro, Kan, Oboge of Nyikidi and his son called Obunde. At this time Nyikidi, the father of Obunde had already died. The Kagwa came to Sakwa. After settling in Sakwa a war between the Kagwa and the Sakwa broke out again because, truth to tell, the Kagwa were instigators of many conflicts. They were very courageous in warfare and enjoyed fighting. But because they were so few they were [3.140.198.43] Project MUSE (2024-04-25 16:38 GMT) 172 SURA YA TISA wachokozi sana. Vita hivyo ndivyo vilivyoua shujaa wa Kagwa aitwaye Obwago Rabuon wa Nyadero na wengine. Hata hivyo Nyadero, baba wa Obwago, naye aliuawa na Walang’o (Wamasai) katika vita vyao nao katika mpaka wa Nyakach na Kano. Wakagwa wanahama Sakwa kwa Vita Wakati Wakagwa walipoingia Sakwa kutoka Imbo Kadimo vita viliwakumbatenanawatuwaSakwawalishirikiananamakabilamengine kuwapiga Wakagwa. Jambo hilo ndilo ilililotawanya watu wa Kagwa sana. Siku moja Wasakwa walipanga njama ya kuwazingira Wakagwa na kuwaua. Lakini mlango wa (ukoo) Kadigol, wao waligundua siri hiyo nao wakahama usiku bila koo zingine za Kagwa kujua. Wakati huo huo watu wa Sakwa wakapata habari kwamba ukoo wa Kadigol, walio na nguvu, wamehama. Wengine wamekwenda Seme, Gem na Uyoma, na waliobaki ni koo za Nyagwala na Yewe, ambao si koo kubwa na hawana nguvu sana. Basi Wasakwa wakapanga jinsi watakavyozingira Wakagwa, nao wakaamua wajigawe sehemu mbili kubwa 1. Sakwa, ukoo wa Nyasmwa, wao walipangwa kwenda kupambana na ukoo wa Wayewe wa Kagwa, na 2. Sakwa, ukoo wa Nyamwanda, wao walipangwa kwenda kuzingira ukoo wa Nyagwala wa Kagwa. Koo hizo za Kagwa ni wale waliopitia mpakani (Mbawa), ndipo balaa hiyo iliwapata. Siku hiyo watu a sakwa waliwaua Wakagwa kiasi cha kuwamaliza. Wale wachache waliobaki walikimbilia sehemu nyingi kuokoa maisha yao; hasa sehemu waliyokimbilia sana ni Alego, Gem na Kisumu na wachache walibaki humo kwa jamaa zao. Ukoo uliobaki bila kuuawa ni ule wa Kadigol waliotoroka mapema wakielekea Uyoma, kikundi cha Kadigol, Oliang’a nyar Miero. Wapo vikundi vitano vikubwa kabisa huko Uyoma hadi leo. Ila wachache sana ndio waliobanduka wakaja hapa Tanganyika kuja kujiunga na koo zingine za Kagwa, nao miji walionao Tanganyika haifiki hata kaya ishirini, nao ndiyo wakina Odede, baba wa Thimotheo Apiyo wa Odede.1 Obwago Ndego alipiga kelele tena, “Twendeni hawa watu wa Sakwa wametuchosha.” Basi pale ikawa na kutokuelewana kati yao wenyewe, na wakaanza kutawanyika ikawa kila mzee au kiongozi wa ukoo, yeye anafuata njia yake na watu wake, hasa wakielekea kwa wajomba, marafiki, au wakwe. Kuna kikundi waliokwenda Uyoma, nao ni: 1. Oboge, 2. Obunde wa Oboge, 3. Muyore wa Obunde, na watu wao. Kuna kikundi kikiongozwa na Obwago Ndego, wao walikwenda Kisumu Odit, katika mji ambayo walioa binti wa Obwago mwenyewe. Na kwa sababu 1 Mzee Achieng’ Odhier. CHAPTER...

Share