In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

PART ONE 143 LESSON 40 TATU AENDA POSTA Vocabulary posta; sanduku la posta post office, post office box (SLP) (P.O. Box ) barua; kuandika barua, letter, to write a letter barua ya ndege; kwa ndege, airmail, by airmail kupata barua, to get a letter kutuma barua, to send a letter kuandikiana barua, to correspond, write each other kujibu barua, to answer a letter stempu; kuweka stempu; stamp(s) to put a stamp tarishi, ma-, messenger(s) kuchukua, kupeleka, to take, to send ngamia; farasi, camel, horses(s) treni; basi, kwa miguu, train, bus, on foot Tatu alikwenda posta kupeleka barua kwa rafiki yake Wambura. Tatu anakaa Tanzania na Wambwa anakaa Kenya. Tatu na Wambura huandikiana barua mara nyingi. Kila mwaka Tatu na Wambura hukutana mara moja Arusha au Nairobi. Mwaka jana Wambura alikuja Arusha, mwaka huu Tatu atakwenda Nairobi. Kabla ya kwenda ni lazima Tatu atangulize barua kumweleza Wambura siku na saa ya kufika. Juzi Tatu alipata barua kutoka Nairobi kwa Wambura. Bila kukawia Tatu alijibu mara moja, alisema, “Mpenzi Wambura, salamu sana. Asante kwa barua yako nzuri. Nimefurahi kusikia 144 SWAHILI MADE EASY umefika salama. Pole kwa safari ndefu.Wewe una bahati, unasafiri kwa ndege, mimi bado sijapanda ndege. Kila mara nasafiri kwa basi au kwa treni. Nikipata fedha mwaka huu nitakuja Nairobi kwa ndege. Nitakuarifu mapema uje kunipokea uwanjani...” Watu wengi wanaandikiana barua siku hizi. Barua zinachukuliwa kwa ndege, kwa treni, kwa basi na hata kwa miguu. Zamani sana huko Uingereza matarishi walikuwa wakipanda farasi kusambaza barua, huko Uarabuni walipanda ngamia, na hapa kwetu walikwenda kwa miguu. ZOEZI LA 49 1. Je,Tatu anafanya kazi posta? 2. Je,Tatu alikwenda posta kufanya nini? 3. Je, rafiki ya Tatu anakaa wapi? Jina lake nani? 4. Je,Tatu alipata barua lini? 5. Barua zinapelekwaje siku hizi? 6. Je, matarishi wa Uarabuni walipanda nini zamani? 7. Je, matarishi wa wapi walikwenda kwa miguu? 8. Je, nani hajapanda ndege,Tatu au rafiki yake? 9. Je,Tatu atakwenda wapi mwaka huu? 10. Je,Tatu na rafiki yake hukutana kila mwaka mara ngapi? Useful Expressions kupeleka simu, kupiga simu, to send a telegram Neno moja ni shilingi moja, one word costs one shilling kutuma fedha kwa simu, to send money by telegram kwa posta, by postal order Nataka kupiga simu I want to call Nairobi Nairobi. [3.128.94.171] Project MUSE (2024-04-19 07:01 GMT) PART ONE 145 dakika tatu ni shilingi Three minutes cost ten shillings kumi. Nipe fomu ya simu. Give a telegram form. Jaza fomu hii hapa. Fill the form here. Weka sahihi yako hapa, Sign your name here. Kuna gundi hapa? Is there gum here? bahasha za rejesta. envelopes for registered letters karatasi za ndege. aerogrammes, Posta kubwa iko wapi? Where is main post office? Posta kubwa iko mjini. It is in town. Unafikaje mjini How do you get there (town) toka hapa? from here? Kuna basi, kituo kile pale. There is a bus, the bus-stop is there lnachukua muda gani How long does it take to get kufika? there? Nusu saa au zaidi dogo, Half an hour or a little more. Nisaidie chenji, Please, some change. ...

Share