In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

PART ONE 125 LESSON 36 KIWANJA CHA NDEGE Vocabulary kiwanja; kiwanja cha ndege, plot, ground, airport ndege; kwenda kwa ndege, bird, aircraft, plane, to go by air kuruka kwa ndege, to fly (by aircraft) kushuka; kutua, to descend, to land kusafiri kwa ndege, to travel by air kupima mizigo, to check mzigo; mizigo, load, loads, luggage sanduku; masanduku, suitcase(s) juu ; juu angani, up, up in the sky anga; angani, sky, in the sky rubani, ma-, pilot(s) wafanyakazi wa ndege, crew kwenye kiwanja cha ndege, at the airport kukaguliwa na polisi, to be checked by the police kuteka nyara ndege, to hijack plane Tatu alikuwa na rafiki, jina lake Wambura. Siku moja Wambura alimwandikia Tatu barua. Katika barua ile alisema,“Salamu, rafiki yangu, nitakuja kwa ndege keshokutwa, tutaonana na kuongea mengi...” Tatu alikwenda kiwanjani kumpokea rafiki yake. Wambura alitoka Nairobi kwa ndege ya asubuhi, waliondoka Nairobi saa mbili na walifika Arusha saa mbili na nusu. 126 SWAHILI MADE EASY Ndege ilipotua, Wambura alitoka pamoja na wasafiri wengine. Tatu alimpokea mizigo yake na kuiweka katika teksi. Njiani waliongea kwa furaha, mara kwa mara walicheka sana. Dereva wa teksi alifurahi pia kusikiliza mazungumzo yao. Kwa kweli ni furaha kuona watu wanaopendana. Walipofika nyumbani kwa Tatu, watoto walikuja kumsalimu mgeni. Mashaka alisaidia kuchukua mizigo na Chausiku aliandaa meza. Sijali alikuwa nje akicheza na wenzake. Mama yake alimwita, akaja mara moja. Jioni Wambura aliwasimulia habari za safari yake ya ndege. ZOEZI LA 44 1. Je, rafiki ya Tatu ni nani? Anakaa wapi? 2. Je, barua ilitoka kwa nani? Ilisema nini? 3. Je, rafiki ya Tatu alifika Arusha saa ngapi? 4. Ndege ilichukua muda gani kutoka Nairobi mpaka Arusha? 5. Je, kwa nini dereva wa teksi alifurahi? 6. Je, Sijali alikuwa wapi mama yake alipomwita? 7. Je, nani alisaidia kuchukua mizigo? 8. Je, Chausiku alifanya nini? 9. Je, nani alisafiri kwa ndege na baadaye kusimulia juu ya safari yake? 10. Je, ndege ilipotua Wambura alifanya nini? Useful Expressions barua ya ndege, airmail. kupeleka barua To send letters by airmail. kwa ndege, [18.118.140.108] Project MUSE (2024-04-19 01:05 GMT) PART ONE 127 kuondoka; ndege To depart, the aircraft has taken off imeondoka, kupokea mgeni, to receive a guest. mgeni alipokelewa The guest was very well received. vizuri sana, kusindikiza mgeni, To see a guest off, to escort. kuaga; kuagana. To take leave off, to part company. ndege kuanguka, Air crash. ajali ya ndege, Air accident. Barua ya ndege Airmail takes one hour inachukua saa moja from Arusha toka Arusha mpaka to Nairobi. Nairobi, kufunga mkanda; To tie the belt, to untie kufungua mkanda, the belt. kuvuta sigareti, to smoke. Msivute mpaka Don’t smoke until we are up tufike angani in the air. Zimeni sigara zenu sasa, Put off your cigarattes now. Mnaweza kuvuta sasa, You may smoke now. Kaeni wima vitini, Stay up right in your chairs. Mnaweza kulala sasa, You may recline now. Je, hupendi safari ya Don’t you like to go by air? ndege? Ninaogopa kusaftri I am afraid to travel in the air. angani, Hakuna sababu No reason to be afraid. ya kuogopa, 128 SWAHILI MADE EASY Ndege karibu itaondoka, The aircraft is about to take off. Hali ya hewa si nzuri, The weather is not good. Kuna mawingu na There are clouds and much fog. ukungu mwingi, Kiwanja kimetanda The airport is covered with fog. ukungu, Kuna mvua pia leo, There is rain also today. Ndege nyingi Many aircraft cannot land zinashindwa kutua because of fog. shauri ya ukungu, Karibu jua litatoka, The sun is about to come out. Ukungu umezidi siku hizi, There is too much fog nowadays. HADITHI Ndege moja ilikuwa angani. Rubani aliwaambia wasafiri, “Mnaweza kuvuta sigara sasa.” Baada ya muda mfupi, alitoa sauti kubwa akisema, “Zimeni sigara zenu upesi, na fungeni mikanda mara moja.” Watu wote waliogopa. Ndege ilikuwa juu ya mawingu, ikaanza kushuka upesiupesi. Chini ya mawingu kulikuwa na ukungu; rubani hakuweza kuona kiwanja cha ndege. Alijaribu kuzunguka, lakini ndege ilizidi kushuka. Mwishowe, alitua shambani. Rubani huyo alikuwa hodari sana. Japo ndege ilikuwa mbovu, lakini alitua salama, hakuna mtu aliyeumia. Ndege ilipotua, wasafiri wote walitoka wakitetemeka. Wote walimshika rubani mkono na kumpa heko kwa uhodari wake. Watu wengi walikuja kuona ajali hii ya ndege. Walishangaa walipoona wasafiri wote salama kabisa. Baada ya saa moja hivi, helikopta ilikuja ikawachukua wasafiri wote. [18.118.140.108] Project MUSE (2024-04-19 01:05 GMT) PART...

Share