In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 89 Huko hafiki Kamange, twaghau fil-biladi91 Matajiri na wanyonge, daima wataradadi Sisikii kifenenge, nimepumzika Hodi! Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Hupenda kumchukuwa, liakhi bin Saidi Hukhofu kuliya ngowa, ni lazima hana budi Tamma nimerufukiwa, nisende na mafisadi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KUMURIYA Msamiati kumuriya jina la ndege mnandi jina la ndege faswiha faswaha; mjuzi au hodari wa kuzungumza au kusema hakuvundi hakuvunji; hakukatalii na akili hapagawa nikapagawa na akili; nikapotewa na akili hilenga nikilenga mithali mfano hazitindi hazimaliziki kucha muhali kuogopa lawama tamkata tindi tindi nitamkata vipande vipande latwifa mpole mtu twagha mtu mwenye kiburi mwili uenele swigha mwili umeenea mapambo Ndiye yeye kumuriya, hapo mbele ya mgandi Faswiha akikujiya, utakalo hakuvundi Mwepesi wa kuridhiya, ni kinyunya hakushindi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa 91 Yaani “mfanya maovu katika miji”. Tamko hili latokana na Qur’ani (Alladhiyna twaghaw fil-bilaad) Aya ya 11 ya Sura ya 89, ambayo yahusiana na Firauni. 90 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kwa maringo na swafawa, hamo katika makundi Ulimi wake haluwa, jozi swafi ya Kihindi Na akili hapagawa, mbwiza hushinda mnandi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa Hilenga sifa mithali, sifa kwake hazitindi Lau si kucha muhali, ngesema ni mwana Hindi Anikanyapo fidhuli, tamkata tindi tindi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa Mtiye katika sifa, ni lubu katika Kindi Tabiya yake latwifa, si jeuri ‘Nenda!’ ‘Sendi!’ Nasabaye ni sharifa, rejesta na kwa hundi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa Tamma ungiye faragha, umpetepete hundi Hulegeya mtu twagha, bwangabwanga huwa fundi Mwili uenele swigha, ni zagao la kizandi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NIRUHUSU TWALIYANI92 Msamiati ayi badru tamama ewe mwezi uliotimia, ewe mwezi mpevu kuchuma kufanya biashara shahreni miezi miwili hapo nendapo sakini hapo ninapokwenda kukaa; hapo nitakapokuwapo atrafu sehemu (za mji); mitaa Ayyi badru tamama, nakuja kaswidiani Kukuarifu nahama, kama utaniidhini Nafika Bopwe kuchuma, kwa muda wa shahreni Niruhusu Twaliyani, nakuaga matembezi 92 Neno “Twaliyani” lina asili ya lugha ya Kiarabu, na lina maana ya “mwanamke mwenye weupe wa rangi ya pera”. ...

Share