In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 87 Hakika ukimshika, mfano wa atwilasi Jamii kalainika, ameghilibu unasi Buruji alozalika, hakuzawa kwa nuhusi Anitosha yeye basi, sitaki mwengine tena Haiba wajihi wake, aliumbwa kwa viyasi Ni kathiri sifa zake, baadhi twazinukusi Kifuwa na shingo yake, maringo kwa kulla jinsi Anitosha yeye basi, sitaki mwengine tena Apendalo tamridhi, milele sitamtusi Simfanyiye gharadhi, asemalo huwa basi Kwa mtu asikaridhi, libasi wala fulusi Anitosha yeye basi, sitaki mwengine tena Tamati mpe umri, Jalla-wa-ala Quddusi Mnusuru na sihiri, aduwi na majasusi Muhifadhi kulla shari, aketi ataanasi Anitosha yeye basi, sitaki mwengine tena ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ RAMADHATIL-’IMADI89 Msamiati nafurahi ghaya nafurahi sana mausufu enye kusifika kwa rukuni mshayadi kwa nguzo imara shamsi jua mirikhi jina la sayari (Mars) utwaridi jina la sayari (Mercury) rihi harufu (nzuri) uturi minal-ali manukato ya hali au kiwango cha juu ambazo si maujudi ambazo hazipatikani (kwa urahisi) mishmishi aina za maua fadhali bora 89 Hapa maana yake ni “nyumba kubwa”. Tamko hili latokana na Qur’ani (Iramadhaatil-imaad), Aya ya 7 Sura ya 89, ambayo yaendeleza fikira iliyoanza kuelezwa katika Aya iliyoitangulia. Katika Aya hiyo ya 6, Mwenyezi Mungu yuwaeleza jinsi alivyowaadhibu watu wa Adi (Iram), ambao walikuwa katika kaumu ya Nabii Hud. Watu hawa walifanya kiburi kwa sababu ya nguvu na madaraka waliyokuwa nayo, “hata wakisema, ‘Ni nani mwenye nguvu kuliko sisi” (Sheikh Abdullah Swaleh Al-Farsy katika tafsiri yake, Qurani Takatifu, Islamic Foundation, Nairobi, (Chapa ya Tano), 1987). 88 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani halitindiki abadi halimaliziki milele wa-ghairuha idadi na nyenginezo zisizokuwa hizo pweke wahidi faridi (mimi tu) pekee; peke yangu wataradadi huenda na kurudi; huzungukazunguka kifenenge mbinja; mruzi ameghilibu unasi amedanganya/ ameshinda watu wote nuhusi nuksi; kasoro; kisirani wajihi uso kathiri nyingi Jama nafurahi ghaya, na kulla siku nazidi Rabbi menijaaliya, ramadhatil-imadi Na rehema yatosheya, ndugu zangu nafaidi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Ah! nimeihamiya, ramadhatil-imadi Mausufu mwasikiya, hiyo jannati shidadi Yatosha yatutosheya, nashukuru hihimidi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Inajengwa kwa nafasi, kwa rukuni mshayadi Kwa nguzo za almasi, lulu na zubarjadi Nuru hushinda shamsi, mirikhi na utwaridi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Huisikiya kwa mbali, rihi miski na udi Uturi minal-ali, ambazo si maujudi Na mishmishi fadhali, asmini na waridi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Fakihati zaujani90 , halitindiki abadi Tini na mizaituni, wa-ghairuha idadi Hula nnachotamani, pweke wahidi faridi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Jamii waitamani, raiya na masayyidi Kwa macho hawaiyoni, wamekwisha jitihadi! Najaliwa Sarahani, kuikiwa makusudi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya 90 Tamko hili latokana na Qur’ani (Fiyhimaa min kulli faakihatin zawjaan) Aya ya 52 ya Sura ya 55, ambayo yaeleza baadhi ya mambo yaliyomo Peponi. Maana ya Aya hii ni: Muna humo, katika kila matunda, namna mbili (na zaidi za kila aina). [3.133.131.168] Project MUSE (2024-04-24 05:14 GMT) Sarahani 89 Huko hafiki Kamange, twaghau fil-biladi91 Matajiri na wanyonge, daima wataradadi Sisikii kifenenge, nimepumzika Hodi! Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya Hupenda kumchukuwa, liakhi bin Saidi Hukhofu kuliya ngowa, ni lazima hana budi Tamma nimerufukiwa, nisende na mafisadi Ramadhatil-’imadi, jama nimeihamiya ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KUMURIYA Msamiati kumuriya jina la ndege mnandi jina la ndege faswiha faswaha; mjuzi au hodari wa kuzungumza au kusema hakuvundi hakuvunji; hakukatalii na akili hapagawa nikapagawa na akili; nikapotewa na akili hilenga nikilenga mithali mfano hazitindi hazimaliziki kucha muhali kuogopa lawama tamkata tindi tindi nitamkata vipande vipande latwifa mpole mtu twagha mtu mwenye kiburi mwili uenele swigha mwili umeenea mapambo Ndiye yeye kumuriya, hapo mbele ya mgandi Faswiha akikujiya, utakalo hakuvundi Mwepesi wa kuridhiya, ni kinyunya hakushindi Amenivunja vipindi, kwa maringo na swafawa 91 Yaani “mfanya maovu katika miji”. Tamko hili latokana na Qur’ani (Alladhiyna twaghaw fil-bilaad) Aya ya 11 ya Sura ya 89, ambayo yahusiana na Firauni. ...

Share