In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

42 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kesho siku ya Kiyama, takallama aydiykum61 Ni hapo penye zahama, tash-hadu arjulukum Swiyaha mwenda lalama, na adhabu fawqakum Innash-shaytwana lakum, ‘aduwwum-mubiyn Tamma mkikasirika, ifaeni dhulmakum! Haiswiri kutanika, mkikokota zubbukum Kumbakumba katamka, hayaatikum wa mamaatikum! Innash-shaytwana lakum, ‘aduwwum-mubiyn ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NANI AJUWAYE PENDA?62 Msamiati mud–hishul– uquli mpoteza akili (kwa amwonaye) katakamali amekamilika puwa fyanda pua shete; pua ya kubabatana; kinyume cha “pua ya upanga” ilaye ila yake; kasoro yake anesa anepa; anyumbuka zenengo (sauti ya) mvumo gonda sauti nene; sauti mbaya piga muunda piga teke kudhumani komamanga himtafuna vifunda nikimbusu michuchu maziwa/matiti makubwa 61 Hizi ni sehemu za Aya ya 65 ya Sura ya 36 (Sura Yaa-siyn) katika Qur’ani: Alyawma nakhtimu ‘alaa af-waahihim wa-tukallimunaa aydiyhim wa-tash-hadu arjuluhum bi-maa kaanuw yaksibuwn, inayohusu habari ya wale watakaokuwa katika moto wa Jahanamu: Kwamba hawatakuwa na njia yoyote ya kukana maovu waliyoyatenda duniani walipokuwa hai, kwani siku hiyo Mwenyezi Mungu ataifunga midomo yao, na badala yake viungo vingine vya miili yao ndivyo vitakavyokuwa vikitoa ushahidi dhidi ya watu hao kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Maana ya Aya hiyo ni: “Siku hiyo tutaviziba vinywa vyao, ituzungumze mikono yao na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma” (yaani madhambi yao). 62 Majibizano haya hayakutungwa siku moja. Kwa hivyo si majibizano ya papo kwa papo. Ifahamikavyo ni kwamba Ruweihy aliliona shairi la Kamange muda mrefu baada ya kutungwa; naye akalitungia jawabu. IngawashairihilililitungwaPembamwanzonimwakarneyaishirini,umaarufuwakeuliendeleakwamiaka mingi, mpaka Bwana Abdurrahman Saggaf Alawy akaja akalipokea kutoka kwa Seif bin Aqida Ahmad Al-Mauly wa Vanga, katika mwaka 1941. Na wakati wa ziara yake huko Pemba, Bwana Abdurrahman Saggaf Alawy alikutana na Ruweihy (ambaye jina lake haswa ni Muhammad bin Juma Kharusy). Baadhi ya wasimulizi waeleza kwamba Kamange mwenyewe ndiye aliyemtia chocha (aliyemchochea) Ruweihy kulijibu kwa namna ya kuuvunja uzuri wa huyo asifiwaye. Shairi hili lilipopatikana kwa ukamilifu ilikuwa ni mwaka 1976. Kamange 43 chanda kidole aqali (kwa) uchache mwanangwa mwana wa watu!; mtoto wa watu!; mtoto wa wenyewe! huwal–haqiri ni mimi mnyonge Banadiri, Bulughi, Burinda majina ya miji libasi nguo uturi manukato mwenda mwendawazimu Kamange: Mud-hishul-uquwli, umuonapo akenda Mzuri katakamali, umbole hakujipinda Alivyo sura jamali, sioni wa kumshinda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Ni mrembo Basha Ali, una nini warerenda? Huyo hakutakamali, kwanza ana puwa fyanda Ndiyo ilaye ya pili, mwendowe wa kujipinda Wacha Basha kujipinda, yahya hashindi mtu Kamange: Akenda hutupa shingo, ajuwa na kujitanda Na jumla ya maringo, sauti kama kinanda Ukimgusa maungo, anesa kama ulanda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Ajuwaje tupa shingo, mtu mfupi kidunda? Sauti kama zenengo, jinsi alivyo na gonda Hajuwi nesa maungo, japo mpiga muunda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu [18.227.114.125] Project MUSE (2024-04-18 08:50 GMT) 44 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kamange: Akiniona huliya, mfano wa njiwa kinda Kudhumani huchezeya, himtafuna vifunda Uso wake qamariya, mwezi ambao wadanda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Akikuona huliya, kwani upate mfunda Ni lipi la kuchezeya, hiyo michuchu mitanda Usowe si qamariya, ana jichwa pandapanda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu Kamange: Kidomo kama kaswiba, ni shida kupita chanda Kidogo hula hushiba, wala hadhofu huwanda Sitaki vinywa mikoba, hashibi ni kama nunda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Kidomoche si kaswiba, aqali ni kumi vyanda Maishaye hatashiba, kama mfano wa punda Wala naye hana hiba, ana tumbo kama kanda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu Kamange: Tachuma kimpa yeye, nakhiyari vaa binda Tena nimnyenyekee, nisimfanyiye inda Nikhuni nimpendaye, mwanangwa asije konda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Chuma ukimpa yeye, awande asiwe ng’onda Hapana amtakaye, ujuwe amekuganda Mrembo umsifuye, aibu zimemtanda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu Kamange 45 Kamange: Sasa nakhofu tembeya, wapenziwe wamlinda Na sasa naazimiya, haja zangu kuzivunda Nikae nnaridhiya, kwake nilale hishinda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Sasa ruhusa tembeya, hadi Bogowa na Tunda Wallahi nakuapiya, hayupo wa kumlinda Sote tumekuwachiya, yakhi anuka kidonda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu Kamange: Tamma huwal-haqiri, silijuwi la kutenda Ningempa Banadiri, na Bulugi na Burinda Na libasi na uturi, na hiba zisingetinda Nani ajuwaye penda, kya yahyal-fuadi? Ruweihy: Tamma mtu khantwiri, hwendaje mfanya inda? Na asiye na nadhari, na umbole kama mwenda Nami hayo sitakiri, mdogo hadhi kupanda Wacha Basha kujiponda, yahya hashindi mtu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ...

Share