In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 25 Niyatili matulubu, twakuomba Subhana Yamvumiye maghibu, kusi na mmande pana Kwa baraka za Habibu, Musa bin Imrana52 Doriya kapatikana, naende mbele afike Tamma ende mwana kwenda, Ilahi ndiwe Rabbana Ende posi ya Uganda, ikamshukiye lana Rabbi haya twayapenda, hima tupate bayana Doriya kapatikana, naende mbele afike ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KWANI MTOTO KITUMBO...?53 Msamiati mtoto kitumbo mtoto mchanga; mtoto mdogo akhuwa ndugu yangu usungo hali ya kuwa mjinga wa mambo yahusianayo na unyago fyuka shuka tambo mtego ndembo tembo; ndovu asadi simba ndimi ni mimi udil–karaha aina ya udi ambao hutafunwa na mtu mwenye ugonjwa wa baridi yabisi kwa ajili ya matibabu huharikisha hutikisa; hufanya (kitu) kikawa na harakati 52 Nabii Musa bin Imran. Katika ubeti huu, Kamange yuwamuomba Mwenyezi Mungu amgharikishe huyo Doriya, kama alivyomgharikisha Firauni na watu wake walipokataa kumfuata Nabii Musa, baada ya kuwalingana kwamba wafuate mafunzo aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 53 “Nilizipata hizi beti nne za shairi hili katika daftari ya babangu, marehemu Mwinyi Alawy. Mwanzo sikujua kama shairi hili ni la kilma na jawabu mpaka baada ya kujuana na Matwar bin Sarahani. Yeye ndiye aliyenieleza kwamba shairi hili lilikuwa ni jawabu ya Sarahani kumtetea mwanawe, Salim bin Hemed. Huyu Salim bin Hemed alikuwa ni mjukuye Kamange kwa nasaba. Yasemekana kwamba Sarahani alimfunzia Salim ende akamtongoze msichana, ambaye Kamange alikuwa ana wivu naye. Kamange alipojua kwamba Salim amfanyia jeuri ya kumtongozea msichana wake, akapandwa na hasira kubwa, kama lionyeshavyo shairi. Kwa bahati mbaya haikuwezekana kuzipata beti zote za shairi hili; kwa hivyo hili halikukamilika. (Abdurrahman Saggaf Alawy) 26 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Ewe Shekhe Sarahani, mbona mwanikaa kombo? Hino ni suhuba gani? Akhuwa mna vikumbo! Ndiyo akhiri zamani, viumbe hapana jambo Kwani mtoto kitumbo, kunyanyuwa fyuka yangu? Kunyanyuwa fyuka yangu, ni usungo ni urombo Akatowa nyama wangu, aliye ndani ya tambo Wanafunzio ni wangu, mbona wanifanya mambo? Kwani mtoto kitumbo, kunyanyuwa fyuka yangu? Salimu bin Hemedi, amejigeuza ndembo Mchana hutaradadi, kwa salamu na hujambo Usiku kama asadi, kwa jisu kuu na fimbo Kwani mtoto kitumbo, kunyanyuwa fyuka yangu? Kama mchezo mzaha, natupigane vikumbo Ndimi udil-karaha, huharikisha mitambo Jina langu simsaha, nala watu kama chambo Kwani mtoto kitumbo, kunyanyuwa fyuka yangu? ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KAMANGE HALI MAKOMBO Akhuwa mwaarifiwa, Pemba mbiu ya mgambo Sarahani wakhusiwa, mwenye kondo za vigambo Bahati nimejaliwa, tangu azali kitambo Kamange hali makombo, ala alichokiwinja Katwa sirambi kiganja, naapa sili makombo Nachaguwa nikiwinja, kilicho sura na umbo Dudu kome talipunja, sichi vita vya kimwambo Kamange hali makombo, ala alichokiwinja Simba ala vya kuwanda, akiyameza matumbo Shekhe ala vya kuvunda, viliwavyo na mabombo Mabigili yawapenda, wachezao kwa urembo Kamange hali makombo, ala alichokiwinja Anadi akilingana, Pemba yote na majimbo Izara kunitukana, jina kanita “mchimbo” Wema wangu aukana, hajali kunila wambo Kamange hali makombo, ala alichokiwinja ...

Share