-
LESSON 39. SIASA YA TANZANIA
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
PART ONE 139 LESSON 39 SIASA YA TANZANIA Vocabulary siasa; mwanasiasa; politics, politicians wanasiasa, kutawala; utawala to rule, govern; administration zamani sana, a long time ago Mwarabu; Waarabu, Arab(s) Mwajemi; Waajemi, Persian(s) Mhindi, Wahindi, Indian(s) Mzungu ; Wazungu, European(s) Mchina; Wachina, Chinese pwani, coast, at the coast kwa ajili ya biashara, on the account of business, trade utumwa; mtumwa, wa-, slavery, slave(s) kukamata, watumwa, to capture slaves biashara ya watumwa, slave trade ukoloni; ubeberu, colonialism, imperialism kiongozi, viongozi, leader(s) uhuru; uhuru na kazini, freedom, freedom and work Afrika Mashariki, East Africa ujamaa; kujitegemea, socialism, self-reliance chama; vyama, association(s), partie(s) kupigania, to fight for 140 SWAHILI MADE EASY Tanzania ni nchi kubwa; iko Afrika Mashariki. Zamani sana Waajemi, Waarabu, Wahindi na baadaye Wazungu walifika pwani ya Tanganyika kufanya biashara. Waarabu walikamata watumwa, walifanya biashara ya watumwa. Wazungu walileta ukoloni na ubeberu Tanganyika Watanzania walipigania uhuru wao. Leo Tanzania ni nchi huru. Viongozi wanasema kila mara “Uhuru na kazi!” Kila mtu ni lazima afanye kazi. Siasa ya ujamaa na kujitegemea ni siasa ya kazi. Lazima Watanzania wote wafanye kazi kwa bidii wapate kujenga nchi yao.Tanzania ina watu zaidi ya milioni arobaini. lna watoto wengi na wazee wachache.Watoto ni mara mbili ya wazee. Ni lazima watoto wote hawa waende shule kupata elimu. Shule nyingi zimejengwa na wananchi. Chama cha Mapinduzi (C. C. M.) kinachotawala. Tanzania inaamini kuwa watu wote ni sawa na kinafuata siasa ya usawa wa watu wote, bila kujali tofauti ya rangi , dini, n.k. Watanzania wote wanajua Kiswahili,lugha ya taifa lao.Watanzania ni wakarimu, na ukifika utafurahia kukaa nao. Ili upate kufurahia safari yako Tanzania, jifunze Kiswahili. Wageni wengi wanaokuja Tanzania wanajifunza Kiswahili; wengi wao wanasema Kiswahili ni lugha rahisi kuliko lugha nyingi duniani. Anza leo kujifunza Kiswahili kwa bidii. Ukitaka kujua Kiswahili safi njoo Tanzania baada ya kumaliza kitabu hiki. Ukifika, jaribu kuongea Kiswahili kila siku bila kuogopa kufanya makosa. [107.23.85.179] Project MUSE (2024-03-19 14:41 GMT) PART ONE 141 ZOEZl LA 48 1. Tanzania iko wapi? 2. Watanganyika walipigania nini? 3. Waarabu walikuja pwani ya Tanganyika kufanya nini? 4. Je,Tanzania ina watu wangapi? 5. Nani alijenga shule nyingi Tanzania? 6. Je, ukitaka kufurahia safari yako Tanzania ufanye nini? 7. Je, ukitaka kujua Kiswahili safi utakwenda wapi? 8. Je,Tanzania kuna ubaguzi wa dini au rangi? 9. Je, kwa nini ni lazima Watanzania wote wafanye kazi kwa bidii? 10. Je, nani alikuja Tanganyika kwa ajili ya biashara? 11. Je, nani anasema, “Uhuru na kazi”? 12. Je, ukifika Tanzania utafanya nini upate kujua Kiswahili safi? Political Terminologies bunge; mbunge, uchaguzi; parliament, member of parliament; elect kuchagua, to choose kugombea kura, to campaign for votes upinzani; mpinzani, opposition, opponent kupita bila kupingwa to be selected without opposition kura; kupiga kura, vote, to vote, cast votes kushinda; kushindwa, to win, to loose maendeleo; mapinduzi, development, revolution kuendelea, to develop, to progress 142 SWAHILI MADE EASY nchi iliyoendelea, developed country nchi inayoendelea, developing country kunyonya; unyonyaji to exploit, exploration kukandamiza, to opresss, oppression ukandamizaji, ukombozi; kukomboa, liberation, to liberate chama cha ukombozi, liberation movement mpigania uhuru, wa- freedom fighter(s) kupigania uhuru wa nchi, to fight for freedom of a country vita vya ukombozi, war of liberation silaha; kuchukua silaha, arms, to take up arms zana za vita, war equipment bomu; bomb mzinga; mizinga, cannon artillery bunduki; risasi, gun, bullet mfungwa wa vita, wa -, prisoner(s) of war mkimbizi, refugee(s) kambi ya (za) wakimbizi, refugee camp(s) kutoa msaada kwa to give aid to refugees wakimbizi, kushambulia; kulinda, to attack; to defend kushindwa; kushinda, to be defeated, to win ushindi; ushindi mkubwa, victory, big victory kuunwaga damu, to spill the blood ...