-
LESSON 38. SHULE YETU
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
134 SWAHILI MADE EASY LESSON 38 SHULE YETU Vocabulary shule, shuleni, school, at school kusoma; kusomea, to read, to read for/to kuandika; kuandikia, to write, to write to/for kujenga; kujengea, to build, to build for/with darasa. ma-. classroom(s) mwanafunzi. wanafunzi. pupil, pupils mvulana; wa- boy(s) msichana. wa-. girl(s) mstari. mi-. line(s) kagua. ku-. to inspect simama. ku- to stand up, stop moving nywele; nywele, hair, clean hair nguo; nguo chafu, dress ; dirty clothes shule ya msingi. primary school shule ya sekondari. secondary school chuo kikuu, university chuo cha elimu, college of education kifaa, vifaa, equipment, materials Shule yetu iko katika kijiji. Kijiji chetu kina watu wengi na wengi wao wana watoto. Katika kijiji chetu kila mtoto anakwenda shule. Shule yetu ina wavulana na wasichana wengi, lakini wavulana ni wengi zaidi ya wasichana. Wako wasichana mia mbili na sitini, na wavulana ni mara mbili yao. Je, wako wavulana wangapi? Bila shaka wavulana ni mia tano na ishirini. Jumla ya watoto wa shule yetu ni mia saba na themanini. PART ONE 135 Kuna walimu wengi pia, wa kike na wa kiume. Walimu wanaume ni mara tatu ya walimu wanawake. Dada yangu ni mwalimu katika shule yetu. Mwaka jana alikuwa mwalimu mkuu. Mwaka huu amekataa kuwa mwalimu mkuu, anasema ni kazi kubwa mno, hapati nafasi ya kuwatunza watoto wake nyumbani. Watu wengi wanafikiri inafaa wanaume tu wawe walimu wakuu kwa sababu wana nafasi zaidi kuliko wanawake, hasa wanawake wenye watoto wadogo. Mwalimu mkuu wa shule yetu ni hodari sana. Watoto wote na walimu wanampenda.Siku moja,aliwaambia watoto wote walete mawe ya kujengea darasa la saba. Watoto walileta mawe mengi.Mwalimu mkuu pia alileta mawe kila siku asubuhi.Watoto waliweka mawe yao pamoja. Baadaye walisimarna mstarini, mwalimu mkuu akawakagua kuona kama nywele, mikono, miguu na nguo zao ni safi.Wale ambao walikuwa wachafu wakaadhibiwa. Watoto wachache wanakwenda shule ya sekondari kila mwaka toka shule yetu.Tuna watoto watatu tu wanaosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,na watano katika Chuo cha Elimu cha Morogoro,karibu na Dar es Salaam. Walimu wetu wanafanya bidii katika kazi yao ngumu ya kuwafundisha watoto wetu maarifa mbalimbali. Mbele ya shule kuna shamba kubwa ambalo hulimwa na walimu na wanafunzi. Kila mwaka wanapanda mbegu mbalimbali na wanapata mavuno mazuri. Shule yetu haina shida ya fedha ya kununulia vifaa vya shule. Sisi wazazi pia tunasaidia katika kazi ya shamba la shule. Kuna ushirikiano23 mzuri kati ya shule na kijiji. 23 Ushirikiano here means good relationship, co-operation, understanding. In question 10 (Exercise 47) the world relationship (or uhusiano in Swahili) refers to ushirikiano (you can lookup the rest of the vocabulary at the back). [54.225.1.66] Project MUSE (2024-03-19 07:23 GMT) 136 SWAHILI MADE EASY ZOEZI LA 47 1. Je, shule yetu ina wasichana wangapi? 2. Je, nani alikuwa mwalimu mkuu mwaka jana? 3. Je, watu wengi wanafikiri nani anafaa kuwa mwalimu mkuu? Kwa nini? 4. Je , kwa nini ni vigumu kwa wanawake kuwa walimu wakuu? 5. Je, kwa nini watoto huleta mawe? 6. Je, kwa nini wanafunzi husimama mstarini mbele ya shule kila siku? 7. Je, mtoto mchafu hufanyiwa nini? 8. Je, watoto wangapi wa shule yetu wanasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam? 9. Je, kwa nini shule yetu haina shida ya fedha za kununulia vifaa? 10. Je, kuna uhusiano gani kati ya shule na kijiji chetu? PART ONE 137 CONVERSATION Useful Expressions kwenda shuleni, to go to school. kurudi toka shuleni, to come back from school. mwalimu yuko shuleni, the teacher is at school. hayuko shuleni, he is not at school. kusoma shule ya msingi, to attend primary school kufanya mitihani, to do examinations kufaulu, kushindwa mtihani, to pass, to fail an examination. mtihani mgumu, rahisi, difficult, easy examination. kupata nafasi, to have time for. have a chance. sina nafasi; kwa leo, I have no time today. kazi ya kilimo, agricultural work. fedha ya kununulia vifaa money for buying school equipment TATU TALKS WITH HER SON, MASHAKA Tatu Je, mtihani ulikuwa mgumu? Mashaka Ndiyo, mtihani ulikuwa mgumu sana. Tatu Je, unafikiri utafaulu? Mashaka Sijui, lakini nilifanya karibu maswali yote. Tatu Je, watoto wote waliona mtihani ni mgumu? Mashaka Ndiyo, kila mtoto alisema mtihani huu ni mgumu sana. Tatu Mwalimu wenu amesemaje juu ya mtihani? [54.225.1.66] Project MUSE (2024-03-19 07:23 GMT) 138 SWAHILI MADE EASY Mashaka Hakusema neno. Alisema tu “Poleni watoto!” Tatu Majibu yatatoka lini? Mashaka Majibu yatatoka mwezi ujao. Tatu Ukifaulu utakwenda wapi...