-
LESSON 37. KAZINI
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
130 SWAHILI MADE EASY LESSON 37 KAZINI Vocabulary kazi; kazini, work, at work kufanya kazi; kwa bidii to work with effort kufika kazini, to report for work kuchelewa kazini, to come late to work kuacha kazi, to stop working, to resign kufukuzwa kazi, to be fired lazima kila mtu afanye everybody must work kazi, mvivu wa kazi, too lazy to work hodari wa kazi, hardworking kutafuta kazi; to look for work kupata kazi, to get a job unataka kazi gani? what type of the work do you want? Kazi yoyote ile, any kind of work, no matter what kind Kulima, kupanda mbegu, to cultivate, to sow seeds Kuvuna mavuno, to harvest, harvest PART ONE 131 Tatu ana shamba kubwa. Anafanya kazi shambani pamoja na watoto wake. Kila mwaka wanapanda mbegu nzuri za mahindi, mpunga, maharage na mihogo. Tatu hapendi mtoto mvivu. Siku moja, Mashaka alichelewa kufika shambani. Mama yake alimwambia, “Ukichelewa tena utalima peke yako wakati sisi tumekwenda nyumbani.”Toka siku ile, Mashaka hajachelewa tena kazini. Watoto wa Tatu wanajua lazima kila mtu afanye kazi.Tatu anafanya kazi kwa bidii, na watoto wake pia wanafanya kazi kwa bidii. Mwaka jana Tatu na watoto wake walipata mavuno mazuri sana. Tatu hana shida ya chakula, watoto wake kila siku wanakula chakula bora.Mara kwa maraTatu huenda sokoni kununua samaki, vitunguu na nyama. Kila siku anawapa watoto wake chakula cha kuchukua shuleni. Jioni wakirudi, wanamsaidia kazi shambani. Mashaka ni hodari sana shuleni. Walimu wake wanampenda sana. Chausiku ameanza kusoma juzi tu. Sijali bado mdogo. ZOEZl LA 46 1. Nani alichelewa kazini siku moja? Tatu alisema nini? 2. Tatu ana nini? Anafanya kazi na nani? 3. Nani alipata mavuno mazuri mwaka jana? 4. Je, kuna shida ya chakula kwa Tatu? Kwa nini? 5. Je, watoto wa Tatu huchukua nini waendapo shuleni? 6. Je, watoto wa Tatu hufanya nini wakirudi nyumbani? 7. Je, kwa nini Mashaka anapendwa na walimu wake? 8. Je, Sijali anakwenda shule? Kwa nini? 9. Je, Chausiku alianza shule lini? 10. Je, nani anafanya kazi kwa bidii? [3.235.199.19] Project MUSE (2024-03-19 02:43 GMT) 132 SWAHILI MADE EASY Useful Expressions kumaliza kazi, to finish work kwenda kazini, to go to work kutoka kazini, to come back from work baba yuko kazini, father is at work baba hajarudi kazini, father has not yet returned from work kuanza kazi, to begin working, to start kufanya uzembe kazini, to be careless at work kuwahi kazini; kuchelewa, to be on time for work, kuchelewa kupoteza; kupoteza muda, to lose; to waste time SHAlRl LA KUSIFU KAZI Vocabulary Shairi, poem kusifu, to praise karani, clerk kupanda, to plant us’ende (usiende), do not go adhuhuri, midday ngazi, step, or staircase mnazi, coconut tree (NBSee also the vocabulary list at the end of this book) 1. Usende mjini kutafuta kazi , Utapoteza muda hiyo ni wazi , Kilimo shambani ndiyo hasa ngazi, Ya maisha bora hata kiangazi, 2. Ukitaka chakula bora shambani, Matunda, mayai , huko ni nyumbani, Asubuhi chai , mayai kinywani, Mchana nyama, viazi , wali jioni. PART ONE 133 3. Utu, maisha mema, na ujirani, Yamejenga huko bila kisirani, Hukai peke daima asilani, Ndugu, jirani mwaishi furahani. 4. Mjini watu hawana ujirani, Hawajuani tarishi na karani, Hamuna jambo wapitana njiani, Hekaheka waenda mbio kazini. 5. Imewatawala fedha mpaka ndani, Wakikosa hamuna raha nyumbani, Usingizi hawapati kitandani, Watafika mpaka huko kiwandani. 6. Nawe shika shauri kaa shambani, Jenga nyumba yako nzuri ya thamani, Utapata mwana umwite Shabani, Uishi vema uwe kwako nyumbani. (for explanation of the poem see the key) ...