In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

PART ONE 119 LESSON 34 TATU SERENGETI Vocabulary nyama, nyama mbichi, meat, raw meat mnyama, wanyama, animal, animals mnyama wa porini, wa-, wild animals mbuga ya wanyama, plain reserved for animal bustani ya wanyama zoo simba, lion tembo, elephant chui, leopard pundamilia, zebra fisi, hyena swala, impala sungura, hare kifaru, rhinoceros kiboko, hippo(s) nyati, buffalo nyani, monkey(s) nguruwe, pig nguruwe mwitu, wild pig Mbuni, ostrich twiga, giraffe 120 SWAHILI MADE EASY Wanyama wa nyumbani Domestic animals mbwa, dog paka, cat mbuzi, goat kondoo, sheep ng’ombe, cow, cattle kuku, chicken punda, donkey farasi, horse Tanzania kuna mbuga kubwa ya wanyama wa porini. Je, unajua jina la mbuga hiyo! Inaitwa Serengeti. Iko karibu na mji wa Arusha. Serengeti kuna wanyama wa kila aina, wakubwa na wadogo, kwa mfano: tembo, twiga, kifaru, simba, chui, nyati, mbuni, swala, na wengine wengi. Ukitaka kuwaona wanyama wote hawa nenda Serengeti. Kila mwaka watu wengi huja Serengeti kuona wanyama. Wanatoka nchi mbalimbali: Ulaya, Marekani, Asia, na nchi nyingine. Tatu na watoto wake walisikia habari za Serengeti. Siku moja, walikwenda kuona wanyama Serengeti. Walipofika Arusha, walikutana na watalii wengi, wakaenda Serengeti pamoja. Tatu alifurahi sana kupata nafasi hii kuwaonyesha watoto wake mbuga hii kubwa ya wanyama. Japo walikuwa ndani ya gari,Sijali aliogopa sana alipoona simba amelala na twiga wakila majani. Mama yake alimwambia, “Usiogope, hakuna hatari.” Mashaka na Chausiku waliongea peke yao, sijui waliongea nini. Nafikiri waliongea juu ya wanyama wa porini. Hii ilikuwa mara yao ya kwanza kuona wanyama wengi namna hii. Walifurahi sana. Jioni, Tatu na watoto wake walirudi Arusha mjini , wakalala kwa shangazi yao. Watoto wake walieleza mambo [3.144.252.140] Project MUSE (2024-04-19 10:56 GMT) PART ONE 121 waliyoyaona Serengeti. Shangazi yao alifurahi kusikia hadithi zao, mwishowe alisema, “Mimi pia nitakwenda Serengeti mwaka ujao mtakapokwenda, au mnasemaje? Watoto walijibu wote pamoja, “Ndiyo, shangazi, twende pamoja; Serengeti ni kuzuri sana. Ni moja ya maajabu ya dunia, au sivyo mama?” Mama yao alikuwa bafuni; hakusikia walichosema watoto wake. Kama angesikia, bila shaka angekubaliana na watoto wake. ZOEZl LA 43 1. Je, Serengeti ni nini ? Iko wapi? 2. Je, watu hufika Serengeti kufanya nini? 3. Je, nani aliogopa simba Serengeti? 4. Je, watalii wanaokuja Serengeti hutoka nchi gani? 5. Je,Tatu alikutana na watalii wapi? 6. Je, nani alisema, “Hakuna hatari?” Kwa nini alisema hivyo? 7. Je,Tatu na watoto wake walilala wapi walipotoka Serengeti? 8. Je, shangazi yao alisema nini? 9. Je, nani alisema Serengeti ni moja ya maajabu ya dunia? 10. Je, nani alikuwa bafuni? USEFUL EXPRESSIONS Je, umepata kuona simba? Have you ever seen a lion? Je, umekwishafika Serengeti? Have you been to Serengeti? Bado sijaona simba, wewe je? I have not yet seen a lion, how about you? Twende Serengeti Let us go to Serengeti to tukaone simba, see lions. Twende Ofisi ya utalii Arusha, Lets us go to the tourist office in Arusha. 122 SWAHILI MADE EASY Je, unapenda kuwinda? Do you like hunting? Sijui kupiga bunduki, I don’t know how to shoot a gun. Sipendi kuwinda, ni hatari, I don’t like hunting, it is dangerous. Ndugu yangu ni My brother is a good hunter. mwindaji hodari, Ana shabaha sana, He/she has a good shot. Ana leseni ya kuwinda tembo, He has a permit to hunt elephant. Siku moja alifukuzwa na One day he was chased by tembo lakini haachi kuwinda, elephant. but he did not stop hunting. Siku moja alikutana na simba One day he met a lion face porini ana kwa ana hakujua toface, he did not know how bunduki yake ilivyoanguka, his gun dropped (from his hand) Kuwinda kunapunguza, Hunting reduces the number wanyama, ijapokuwa of animals, even though they wanazaliana reproduce themselves Zamani dunia iijaa Formerly the earth was full wanyama, of animals lakini leo wamebaki But today only afew remain wachache tu Nyama ya nguruwe Meat from wild pigs is good, mwitu ni nzuri, lakini but the meat from impala is nyama ya swala ni better nzuri zaidi. ...

Share