-
LESSON 32. BARABARANI
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
PART ONE 113 LESSON 32 BARABARANI Vocabulary mume (wa), husband, (her) lami, tarmac dereva, driver barabara, barabarani, road, on the road gari; magari, car, cars kuendesha, to drive kusimama; kusimamisha, to stop, to make stop kukimbiza gari. drive fast tope, matope mud utelezi, kuteleza, slippery, to slip mvua, rain, to rain kukwama, kusukuma, to get stuck, to push kupanda, kushuka, to climb up, to descend kwenda kwa gari, to go by car Amina, dada yake Tatu, anafahamu kuendesha gari. Mumewe ana gari jipya aina ya VW. Amina ni dereva hodari, haendeshi mbio, anajua kuwa kukimbiza gari ni hatari. Ukienda kwa gari lake utafurahi, hutaogopa. Siku moja, Amina alikwenda shambani kwa gari. Njiani aliuliza habari za barabara, kwa sababu mvua ilinyesha usiku. Madereva wengine walimwambia njia ilikuwa mbaya sana, yenye matope mengi na utelezi. 114 SWAHILI MADE EASY Basi, Amina aliendesha polepole sana, Alikutana na lori moja. Dereva wa lori alikuwa akiendesha mbio. Amina alikwenda pembeni kumpisha, na hapo alikwama vibaya sana. Kwa bahati lori lile lilikuwa na watu wengi wenye nguvu.Walisaidia kusukuma gari la Amina. Alipotoka katika matope, Amina alifurahi sana. Alisema,“Asanteni sana,ndugu.Sijui ningefanya nini peke yangu.” Watu wale walimsifu Amina kwa uhodari wake.Walisema,“Dada, wewe ni dereva hodari, lakini barabara hizi hazina dereva hodari, kila dereva hukwama mara kwa mara. Kukwama ni desturi katika barabara zetu kwa sababu hakuna/hazina lami. ZOEZl LA 41 1. Je, kwa nini Amina alikwama? 2. Je , nani alimsaidia kusukuma gari lake? 3. Je, kwa nini ni desturi kukwama katika barabara zetu? 4. Je, nani alikwenda mbio? 5. Je, nani ni dereva hodari? Amina au dereva wa lori? 6. Je, Amina huendesha mbio? Kwa nini? 7. Je, kwa nini Amina aliuliza habari za barabara? 8. Je, Amina alipata habari gani za barabara? Useful Expressions Petroli, stesheni ya petrol, petrol, petrol station nipe petroli lita kumni, give me 10 litres of petrol hebu, angalia oili, check the oil pima upepo, check the pressure (of tyres) jaza upepo, fill in the tyres kuna pancha, there is a puncture [100.25.40.11] Project MUSE (2024-03-19 06:57 GMT) PART ONE 115 ziba pancha hii, fill this puncture hakuna pancha; no puncture, valve leakage valvu inavuja, gari limeharibika, the car is out of order tengeneza gari, repair a car kuegesha gari, to park a car pita kushoto, kulia, keep left, right njia ina matope sana, the way is very muddy nenda polepole, go slowly weka cheni, vingine hupiti, put chains; otherwise you won’t pass ni hatari; kuna hatari, it is dangerous; there is danger gari haliwaki; limewaka, car does not start; it has started washa gari; zima gari, start the car; switch off ...