-
LESSON 30. TATU AENDA SOKONI
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
106 SWAHILI MADE EASY LESSON 30 TATU AENDA SOKONI Vocabulary soko, sokoni market, in the market place mji, mjini, town, in the town njia, njiani, way, on the way hasi, mabasi, bus, buses basi, so, then, enough, stop kutuma, kutumwa to send, to be sent peke yangu, peke yako n.k. I alone, you alone, etc. kupenda, kupendana, to love, to like, to love each other kukosa; kosa, makosa, to miss, to make mistake, a mistake, mistakes nafasi; wakati, opportunity, time kuongea, to talk, converse kusindikiza, to accompany, escort sababu; kwa sababu, cause, because Tatu alipokuwa mtoto alikuwa na rafiki jina lake Chenga.Tatu na Chenga walipendana sana. Kila siku walikwenda shuleni pamoja, walicheza pamoja.Siku moja Tatu alitumwa na mama yake sokoni. Njiani alikutana na Chenga, wakaamkiana hivi: PART ONE 107 Chenga: Jambo (hujambo) Tatu? Tatu: Sijambo, je, wewe hujambo? Chenga: Mimi sijambo kabisa, wewe je? Tatu: Usiwe na shaka, mimi ni mzima tu. Chenga: Ni furaha kubwa leo kukutana nawe peke yako saa hizi. Unakwenda wapi? Tatu: Ninakwenda sokoni, mama amenituma peke yangu leo. Chenga: Je, nikusindikize? Sina kazi, nitafurahi kwenda nawe. Tatu: Ukitaka twende, Naogopa kwenda peke yangu. Chenga: Ni bahati kwangu kupata nafasi hii. Tatu: Bahati gani? Mbona tunaonana kila siku? Chenga: Ndiyo, lakini leo ni tofauti na siku nyingine. Tatu: Tofauti gani? Mimi naona sawa tu kama jana na juzi na siku zote. Chenga: Iko tofauti , nitakwambia sasa hivi. Twende tu. Tatu: Haya, niambie basi, kitu gani hicho? Siri, au nini? Chenga: Usiwe na haraka, nitakwambia tu, ngoja kidogo. Tatu: Ningoje nini? Niambie tu, niko hapa, sitakukimbia. Chenga: Nilitaka kukwambia tangu siku nyingi , lakini sikuwa na nafasi. [54.85.255.74] Project MUSE (2024-03-19 09:56 GMT) 108 SWAHILI MADE EASY Tatu: Mbona unazidi kuzunguka tu wala husemi chochote cha maana. Chenga: Ni hivi, ningependa wewe na mini, tukisha kuwa wakubwa tuoane, unasemaje? Hupendi kuwa mke wangu wa maisha? Tatu: Maneno yako hayana maana, kama umekosa la kusema heri kunyamaza. Chenga: Najua huwezi kukubali mara moja, nenda ukafikiri polepole. Tatu: Sina cha kufikiri, inafaa tuongee mambo mengine. Unaona basi lile? Chenga: Twende upesi, tutachelewa, mabasi hapa ni shida sana siku hizi. ZOEZl LA 39 1. Tatu alikutana na nani alipokwenda sokoni? 2. Nani alisema, “Tofauti gani ?” 3. Nani alisema, “Kitu gani hicho?” 4. Nani alimsindikiza Tatu? 5. Nani alisema, “Maneno yako hayana maana?” 6. Nani alisema, “Inafaa tuongee mambo mengine?” 7. Nani alisema, “Ni bahati yangu?” 8. Chenga alimwambia nini Tatu kuhusu kuoana? 9. Je, mabasi ni rahisi au ni shida kuyapata? 10. Je,Tatu alikuwa mtoto au mtu mzima wakati huo? PART ONE 109 USEFUL EXPRESSIONS Bei gani? What is the price? Machungwa haya ni These oranges are fifty cents each thumni kila, moja na yale pale ni and those there are thirty cents senti thelathini, each Nipe matano ya thumni, Give me five for fifty cents each Ndizi, je, bei gani? What is the price of the bananas? Ndizi ni nne shilingi, Bananas are four for a shilling Mbona ghali hivi? Why are they so dear? Ndiyo bei yake situ hizi, This is the price nowadays. Ebu, nipe nyanya mbili, Please give two tomatoes Ni bei gani jumla? What is the total price? Nipe shilingi kumi, Give me ten shillings Tatu, bado unanunua? Tatu, are you still buying? Nimemaliza, twende, I am ready, lets go. Vitu vimepanda bei! Things have become so expensive! Ndugu yangu, sijui Oh dear, I don’t know what we tutafanya nini sasa ? should do now? Sisi watu wadogo tuna We people of low income are in taabu, kweli trouble, indeed! Basi lile, linakuja, There comes the bus. Kwa heri, dada, Bye bye, dear sister ...