-
LESSON 29. TATU21 NA WATOTO WAKE NYUMBANI
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
100 SWAHILI MADE EASY LESSON 29 TATU21 NA WATOTO WAKE NYUMBANI Vocabulary nyumbani, at home shuleni, at school chakula bora, good, nourishing food yai, mayai egg, eggs maziwa, milk mboga, vegetable mchele, wali rice (cooking rice) matunda, fruits (sing. tunda, fruit) -bichi, unripe, uncooked -bivu, ripe kuiva, to be ripe, to be cooked safi, clean usafi, cleanliness chafu, dirty, dirty kukataza, to forbid karibu na, near, nearby mbali ni, far away from ugonjwa, magonjwa, sickness, diseases japo, although (also ijapokuwa, ingawa, ingawaje) Tatu ni mama. Ana watoto waTatu Mashaka, Chausiku na Sijali. Tatu anakaa shamba pamoja na watoto wake. Ana shamba la 21 In these stories, Tatu appears without a husband; that should not worry you. PART ONE 101 matunda na mboga. Tatu anawapa watoto wake chakula bora kila siku: mboga, mayai, matunda, samaki, viazi, mchele/wali, maziwa, nyama, n.k. Siku moja Tatu alimwona mtoto wake, Mashaka, akila matunda mabichi, akamkataza, kwa sababu si mazuri.Tatu alichukua tunda moja zuri akampa Mashaka. Mtoto huyo alifurahi sana, akasema, “Asante, mama.” Siku nyingine Tatu alikwenda mjini pamoja na mtoto wake, Chausiku. Njiani Chausiku alipata kiu akataka kunywa maji ya mtoni. Mama yake alimkataza akisema, “Maji ya mtoni si safi kwa kunywa, yana vidudu vya magonjwa mbalimbali. Ngoja tufike nyumbani nitakupa maji safi” Japo Chausiku alikuwa na kiu sana hakunywa maji yale, alingoja mpaka walipofika nyumbani. Tatu anawalea watoto wake vizuri; anawafundisha kwa maneno na kwa vitendo pia.Tatu ni mama mwema. ZOEZl LA 37 1. Je,Tatu ana watoto wangapi? Taja majina yao. 2. Je,Tatu anakaa wapi? Anafanya nini? 3. Je, vyakula gani ni bora? 4. Je, nani alikula matunda mabichi ? Tatu alifanya nini ? 5. Je, mtoto alisema nini alipopewa tunda zuri na Tatu? 6. Je, kwa nini Tatu alimkataza Chausiku kunywa maji ya mto? 7. Je, Chausiku alifanya nini alipokatazwa kunywa maji ya mto na mama yake? 8. Je,Tatu ni mama mwema? Kwa nini unasema hivyo? 9. Je,Tatu alikwenda wapi na Chausiku? 10. Je, maji ya mto ni safi kwa kunywa? Kwa nini? [54.157.61.194] Project MUSE (2024-03-19 11:14 GMT) 102 SWAHILI MADE EASY NYUMBANI : USEFUL EXPRESSIONS kutandika kitanda, to make a bed kupangusa meza, to dust a table kuandaa meza, to set a table fungua mlango, dirisha, open the door, the window funga mlango, dirisha, shut the door, the window kufua nguo chafu, to wash dirty clothes kupiga pasi nguo, to iron clothes kupiga deki, to wash the floor weka chakula mezani, put food on the table kuona njaa, kiu, to be hungry, thirsty kusafisha vyombo, to wash dishes HADITHI Vocabulary chuma matunda, pick fruits jikoni, in the kitchen nyani, a baboon ogopa be frightened mayowe yells hodari brave fimbo stick Tatu alikwenda shambani kuchuma matunda. Alipofika aliona mengine yameiva na mengine hayajaiva. Dada zake, Bahati na Amina, walitaka matunda. Walichuma matunda yote, mabivu na mabichi. Matunda mabichi waliyaweka jikoni yaive, matunda mabivu waliyala palepale. Walikuwa na njaa. Walipokuwa pale shambani alitokea nyani mmoja mkubwa. Tatu na dada zake PART ONE 103 waliogopa sana. Walikimbilia nyumbani wakilia, “Nyani, nyani! “Waliposikia mayowe hayo, Mashaka na dada zake, Chausiku na Sijali,walitokanje.Mashakaalikuwakijanahodari.Alichukuafimbo akaenda shambani kumfukuza nyani yule. Nyani yule alipomwona Mashaka anakuja na fimbo, akakimbia, akaingia porini. ZOEZl LA 38 1. Je , nani alichuma matunda? 2. Je, matunda yote yalikuwa mabichi ? 3. Je,Tatu na dada zake waliogopa nini? Walifanya nini ? 4. Kwa nini Tatu na dada zake walikula matunda shambani? 5. Je , nani alimfukuza nyani? 6. Je, nyani alikwenda wapi? [54.157.61.194] Project MUSE (2024-03-19 11:14 GMT) 104 SWAHILI MADE EASY AMINA NA MPISHI WAKE JIKONI Vocabulary jiko, jikoni, kitchen, in the kitchen kijiko, vi- spoon(s) umma, nyuma fork(s) kisu, vi- knife, knives sufuria, metal cooking pot sahani, plate(s) kikombe, vi- cup(s) chai, sukari,kahawa, tea, coffee sugar siagi, jibini, butter, cheese mkate, bread asali, honey chumvi, salt Amina Mpishi, leo unapika nini? Mpishi Nitapika wali na samaki, najua wewe huli samaki, nitakupikia nyama. Amina Vizuri sana, Je, wageni wote wanakula samaki, umewauliza? Mpishi Hapana, sikuwauliza, ngoja nitakwenda kuwauliza sasa hivi. Amina Fanya haraka, sasa ni saa tano, tunakula saa ngapi leo? Mpishi Usiwe na wasiwasi chakula kitakuwa tayari mapema kama kawaida. PART ONE 105 Amina Haya nenda, fanya kazi zako, ukitaka msaada niite, unasikia. Mpishi Ndiyo mama. CHUMBA CHA KULALA “THE BEDROOM” Useful Expressions chumba, vyumba, room, rooms chumba cha kulala, bedroom kulala, to sleep, to lie down kuamka, to get up, wake up...