In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

8 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani kwa Maibadhi sigara ni haramu, basi hana utukufu na akizidi kumchokoza moto utashika ndifu. Haya yalikuwa majibizano makali; na baada ya kupita miaka tisiini na mbili tokea kufa Kamange, yanaonekana ni kama ugomvi. Bali hii ndiyo iliyokuwa hali ya washairi wa siku hizo. Kulikuwa na mwimbaji wa Kiamu aliyeimba: Usione mashariya, ya watu wao kwa wao Tahadhari na kungiya, katika baina yao Mbuzi na ng’ombe wamoya, mtu mbali ni kondoo Hata Sarahani na Kamange walikuwa hivyo hivyo; kama alivyosema Sarahani katika lile shairi la kumlilia Kamange: Twali tukitukanana, watu wasitudhaniye Kama hawa wapatana, ya ndani tusiwambiye Kufurahisha fitina, kusudi watuzomee… Ushindani huo ulikuwa ni ushahidi wa usheha wa Kamange. Bin Khatoro aliwaambia: Napita nikiwahani, wandike kaditamati Khalifa wake ni nani, akae juu ya kiti? Acheze na Sarahani, iwane miti kwa miti Kamange kenda kaputi, masikini Basha-Ali MUWACHENI ANIGHURI Msamiati limenighumisha limenilemea; limenielemea anighuri anizuzue dari-madari (kwa) wingi badii jamali mzuri kupita kiasi; mzuri sana kudahadari kutatizika; kuduwala vungevunge ovyo ovyo khantwiri kitu kibaya; mtu mbaya (kwa tabia) hana pezi / hana tenge hana kasoro; hana ila; amepambika mdawari kila upande; pande zote qamari mwezi kaswiba nzumari (hapa kwa maana ya mdomo usiokuwa mpana) tuyuri ndege Kamange 9 khatwiri moyo durari lulu nyingi teketeke laini ufizi nyama iliyomo mdomoni inayoshikilia meno ya juu na ya chini; masine siwadhakhiri siwaingilii (katika mambo yao) kamzaini amempa uzuri (wa umbo) halikujisiri halikujificha alimswawiri alimpa sura (nzuri) fyuka mti (wa mtego) ufungiwao uzi au ukambaa wa mtego ulimbo mtego bilaili wa nahari usiku na mchana latwifu mpole katwa katu; hata kidogo ushari ugomvi awanakidi awatia kombo; awatia ila; awaumbua watahayari wanaona haya ghusnu-banni kitanzu (cha mti) kilicho laini impendeze suduri kifua kimempendeza khaili nyumbu anapokwenda mughari anapokwenda kwa maringo (vitani) kudhumani (ma)komamanga dumu hazitaghayari daima hazibadiliki nastajiri naona raha maqamu (kwa) kiasi bashari binadamu tumbo lake mudhmari tumbo lake (ni) jembamba kwa alfu msayari kwa hatua ndefu; kwa urefu mikando vinoo vya dhahabu au vya fedha ahmari nyekundu kyamburi koleo aini-l-huri hurilaini kijaa jiwe la kusagia ajirenga anaringa; ajitwaza rihi harufu (nzuri) masafatul qaswiri masafa mafupi [3.21.100.34] Project MUSE (2024-04-20 05:19 GMT) 10 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani firashi tandiko maguu qumashi matege bairi ngamia yaumun-nushuri siku ya majuto; siku ya Kiyama, ambapo binadamu watahukumiwa na Mwenyezi Mungu kwa waliyoyatenda walipokuwa hai duniani. Waliotenda mema na kujiepusha na maovu, kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (kulingana na mafunzo ya Uislamu), watalipwa mema; na waliotenda maovu watalipwa maovu na kuadhibiwa. Kwa hivyo, siku hiyo ni siku ya majuto kwa wale waliotenda maovu. wa-qina adhaban-nari na utuepushe na adhabu ya Moto wa Jahanamu jududi na duhuri sasa na wakati ujao Kweli pendo ladhiisha, khususwa likikithiri Nami limenighumisha, mwenzenu sina khiyari Na hivi lanikondesha, kwa yeye himfikiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali28 Ndiye Badii Jamali, hapa hana chanjari Kwa naswaba na aswili, lubbu katika fakhari Kwa iqibala na mali, ndiye jarra majururi Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Swifaze zimemweneya, jamii dari-madari Yoyote kimtokeya, hawachi kudahadari Ilahi kamja’liya, kwa jamali na uzuri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Kichwa chake mviringe, ndiyo mwanzo wa khabari Hakuumbwa vungevunge, kama hawa khantwiri Hana pezi hana tenge, sawa sawa mdawari Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Ibara ya nywele zake, laini kama hariri Nadhani kiyasi chake, ni dhiraa na shubiri Mufti wa wanawake, ni huyu amedhihiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Macho mfano wa dira, kulla upande hujiri Hudhani saba sayara, ndizo nyota mashuhuri Anga hushinda Zuhura, hudanda kama qamari Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali 28 Hili ni jina la mwanamke aliyemo katika hadithi za Alfu Lela-u-Lela, anayesifiwa kwa uzuri wake. Kamange 11 Midomo kama kaswiba, kupigiya nzumari Kula kidogo hushiba, hudona kama tuyuri Namtaka mwenye twiba, anipumbaze khatwiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Basi hikaya acheke, meno yashinda durari Midomoye teketeke, ufizi kama johari Banati nawaghasike, kwa haki siwadhakhiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Usowe nuru hucheza, kamzaini Qahari29 Japo pakiwa na kiza, hilo halikujisiri Nyusi zikampendeza, puwa ilivyo kadiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Nyusi zimetiya kombo, Jalla alimswawiri Zatosha kuwa ni chambo, au atakuaziri! Wacha fyuka na ulimbo, hunaswa mwinyi hadhari Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Macho yake asinziya, bilaili wa nahari Manukato anukiya, haliudi na ambari Harufu ikikujiya, miski na kaafuri Muwacheni anighuri, ndiye Badii Jamali Uzuri kama Yusufu30 , au Siti-l-Buduri31 Moyo wake ni latwifu, katwa hajuwi ushari Niacheni nimsifu, nikidhi yangu nadhiri Muwacheni anighuri, ndiye Badii...

Share