In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

108 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kamange: Tammati hilo jawabu, ulimi nautwaliqi Maneno sikuharibu, nimetunga nikinaqi Haishi yetu harubu, ka raadi wa bariqi Njoo Jazirati-Waqi, nikupe kisicholiwa ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ MLANGILANGI NA MKADI106 Msamiati nenda maji kwa matangi ninakwenda kuchota au kuteka maji kwa wingi rihiye harufu yake (nzuri) matuwa matuta muhanuni aina ya maua manqudi hutiwa kasoro naatunde naachume shati usiku laili sharti/ mpaka usiku sana tumbaye tumba yake zengeli pori; msitu hustakidhi muradi hukidhi haja; hutimiza haja majura wapumbavu; wajinga agonjwae anayekuwa mgonjwa; auguaye dum daima Sarahani: Napata mlangilangi, acha moyo utuliye Fufuni na hadi Ungi, hapana aupataye Nenda maji kwa matangi, mwenyewe niutiliye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa 106 Amenieleza Bwana Matwar bin Sarahani kwamba babake alipolitunga shairi hili hakudhani kuwa atatokea mtu alijibu. Na washairi wote wakubwa waliokuwako wakati huo hawakulijibu, kama alivyotarajia Sarahani. Lakini mwanafunzi mashuhuri wa Sarahani, Mswanifu bin Athmani, akalijibu. Yasemekana kwamba kitendo hiki kilimkasirisha sana Sarahani; naye akamwita Mswanifu nyumbani kwake. Alipokuja, akamkaripia sana na kumuonya kwamba asifanye tena jeuri za namna hii, kwa sababu yeye Sarahani ni babake mlezi, na ni mwalimu wake na shekhe lake. Kwa hivyo haimstahilii Mswanifu kuingia ugani na kucheza ngoma na babake. Hatimaye, Mswanifu aliangukia na kuomba mswamaha. Sarahani akamswamehe, na uhusiano wao ukaendelea kama kawaida. (Abdurrahman Saggaf Alawy) Sarahani 109 Mswanifu: Muhibu mlangilangi, sikuuona sifaye Harufu hata si nyingi, ni kiyasi kadiriye Rihi afadhali yungu, kwa mtu achagawaye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Yashinda yote mauwa, unabakiya pekeye Miafu nimeing’owa, sipendi kwangu ikaye Bure kuweka matuwa, mara hwisha harufuye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Haukushinda mauwa, kwa rihi wala suraye Mkadi kufadhiliwa, mtu nashindana naye Hikaya ukivaliwa, hutwibu asikiyaye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Si mkadi si rihani, mtu asinitajiye U sawa na muhanuni, manqudi avaaye Labda wa Micheweni, kwa kujaliza ndeweye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Utungiwapo rihani, huwa ni bora rihiye Daliya na zafarani, kidogo atojezeye Japo kongwe la zamani, hutwibika maradhiye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Mkilwa usifiwao, si kweli usisikiye Huamsha walalao, hutajwa kwa bahatiye Kwa mimi ni radhi nao, naatunde atakaye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa [3.133.79.70] Project MUSE (2024-04-24 04:46 GMT) 110 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Mswanifu: Hata mpesi mkao, umefanana milaye Hudhani wasema ndio, kwa harufu na haliye Mauwa ya mti huo, sisi usitusifiye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Mauwa ya mshembeli, ila yake niwambiye Shati usiku laili, shuwari kusipepeye Kukicha huwa batwili, ni lazima ulegeye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Mkadi umefadhili, sifa rihi usikiye Kwa kukutowa akili, kiifumbuwa tumbaye Huwa katika zengeli, hupenda ufuwatiye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Yasimini na waridi, yana ila ajuwaye Harufu yake baridi, sharuti ukurubiye Na utakapo zaidi, afadhali marashiye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Amma rihi ya mkadi, japo kuwa mtu siye Hustakidhi muradi, kuitwibu nafsiye Kwa kunuka ni ashaddi, awali na akhiriye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Uwa la mchungwa bora, watu wasema; si miye Ni baadhi ya majura, si mtu na akiliye Kwa kulla mtu fukara, hukirimu kwa mbogaye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Wajuwa mauwa bora, lakini ndiyo kiweye Mkadi hauna jora, mengine usinambiye Sarahani 111 Harufu haishi mara, haichuki asiliye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Wangapi wataradadi, waitafuta mbeguye Hawajakidhi muradi, hupata ajaliwaye Mwenye hadhi na suudi, kama Khamisi na miye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Ambao wataradadi, wambiye waje watwaye Kwangu miye maujudi, nitampa atakaye Naihamisha kusudi, shamba isinifujiye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Amma liwapo nyumbani, moja liso zaidiye Ukumbini na chumbani, hughasi kulla ajaye “Dada ni mafuta gani, unigawiye na miye?” Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Muhibu wasema nini, afadhali unyamaye! Mkadi huwa mwituni, asiwe auonaye Na apitaye njiyani, takuwa kimayemaye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Amma naliwe kichwani, nyweleni likaukiye Lisukiwe behedani, alifunike bibiye Suuri na zafarani, humpoza agonjwaye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Auvaapo shingoni, mpenzi umpendaye Suluti na behedani, humpoza agonjwaye Huwa arusi yakini, kuimba na hoye hoye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote [3.133.79.70] Project MUSE (2024-04-24 04:46 GMT) 112 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Sarahani: Taukimu mti wangu, dum niupaliliye Ahadi umri wangu, wala nisiondokeye Japosema walimwengu, hasikii apendaye Mlangilangi rihiye, unafadhili mauwa Mswanifu: Mti huo miye kwangu, wala sinihadithiye Mimi na mkadi wangu, naona manufaaye Hunondokeya uchungu, hufurahi anunaye Mkadi bora rihiye, hushinda mauwa yote Sarahani: Tamati sitaondoka, watu wasikaribiye Tapanda nikijipaka, hichezeya matawiye Msikiye nikinuka, mahasidi wadodeye Mlangilangi rihiye...

Share