In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 101 Ziwapi zamani zetu, za Maliki Dhwirghamu Zenyi neema na vitu, raiya kutanaamu Wanaondoka wenzetu, watilkal-ayyaamu104 Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Ni duwa ya Mukhtari, kutuombeya kaumu Dhambi zinavyokithiri, Rabbi angetunaqimu Nchi angezibadhiri, mfano wa Saidumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Tamma ifikishe hadi, yaa Muhyil-idhwamu105 Ahudhuriye Muhudi, ustakimu Wisilamu Uondowe ufisadi, ulio Makka na Shamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ YAKHE NNA HAJA NAWE Msamiati ilaa Shekhe -l-muhibbu kwa Shekhe mpenzi waswalaka -l-kitabu yamekufikia maandishi; imekufikia barua sallamahu -l-Mannani min jamii -l-hussadi Mwenyezi Mungu akulinde/akunusuru na mahasidi wote takuauni atakusaidia asadi simba khaibani ukosefu nastadhaafu nanyongeka; naona unyonge 104 Hiki ni kipande cha Aya ya 140 ya Sura ya 3 ya Qur’ani: ... Watilkal-ayyaamu nudaawiluhaa baynannaas ...; yaani “... Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zamu...” Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anawakumbusha Waislamu waliopigana dhidi ya Makureshi katika Vita vya Uhud (katika mwaka 625 wa Hijra, na ambapo Waislamu walishindwa kutokana na baadhi ya wapiganaji Waislamu kwenda kinyume na maagizo waliyopewa na jamadari wao, Mtume Muhammad) kwamba majeraha na misukosuko mingine waliyoipata wakati wa vita hivyo, na maadui zao pia yamewafika hayo (katika Vita vya Badr, vilivyopiganwa mwaka mmoja kabla, na ambapo Waislamu walishinda). Yaani hivyo ndivyo maisha yalivyo: Leo kwa mwenzako, kesho kwako - mambo kwa zamu. 105 Mwenye kuihuisha mifupa (baada ya kuchakaa), yaani Mwenyezi Mngu. Tamko hili limetumiwa katika Qur’ani. Kwa mfano katika Aya ya 78 ya Sura ya 36 (Sura Yaa-siyn), ambayo yahusiana na yule asiyeamini kwamba binadamu watafufuliwa na Mwenyezi Mungu baada ya kufa: Wa-dhwaraba lanaa mathalan wanasiya khalqahuw; qaala: Man yuhyil-idhwamaa wahiya ramiym. Yaani Mwenyezi Mungu yuwasema, “Na (mtu huyo anayekadhibisha kufufuliwa) akatupigia mfano na akasahau kuumbwa kwake (kwa manii) akasema , ‘Nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagikasagika?” 102 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Pepo njema muq-adi Pepo njema ya kukaa (milele) kabiri na auladi wakubwa na wadogo jamii–l–hunudi jamii ya Wahindi na kafa wote abidi na viumbe wote aliyefanidi aliyepata mambo mazuri; aliyepata faida ya mambo aj–wadi watu makarimu midadi wino sanati thalatha miya, na thinaashara zaidi zaidi ya miaka mia tatu na kumi na mbili Ilaa Shekhe-l-muhibbu, Thiqati bin Saidi Waswalaka-l-kitabu, fahamu bin Rashidi Sikusahau nasabu, Jahadhmy yako jadi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Sallamahu-l-Mannani, min jamii-l-hussadi Inshallah takuauni, utishe kama asadi Warejee khaibani, wajao kwa ufisadi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Baada nakuarifu, usuli siwe na budi Hima nastadhaafu, nakweleza makusudi Mwito usiukhalifu, sasa hivi utarudi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Salamu ni yako wewe, na rehema ya Wadudi Na baraka uzidiwe, nakuombeya Sayyidi Na Akhera ukatiwe, Pepo njema muq-adi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Nawe usiponijiya, wanikasiri fuadi Ninacho kichaka ghaya, kimeniudhi shadidi Ndicho nnachokwitiya, kwa shime najitahidi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Salamu alaikumu, kabiri na auladi Sulemani na Salimu, na jamii-l-hunudi Punja na Muki Kasimu, na kafa wote abidi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe [18.117.107.90] Project MUSE (2024-04-24 00:21 GMT) Sarahani 103 Wakatabahu shairi, khaswa aliyefanidi Alhakiri-l-fakiri, Sarahani aj-wadi Huwa ni Bunu Matwari, hapakuwa msaidi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Tarikhi nimebaini, kwa kalamu na midadi Khamsa wa ishirini, shahari-l-mardudi Mwezi ni wa Ramadhani, almubaaraka suudi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe Sanati thalatha miya, na thinaashara zaidi Na alfu kutimiya, Hijra ya Muhammadi Yafaa kumswaliya, swallaLlahu Ya Sayyidi Usuli ndio muradi, yakhe nna haja nawe ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NATAKA KISICHOLIWA Msamiati nimetanakali nimeondoka makhluqi binadamu tanabuhi yaa juhuli zinduka ewe mpumbavu hahiliki nikahiliki; nikaangamia umeshteli umeshikwa na maradhi ya baridi; umeishiwa; umeharibikiwa na mambo nastadhiqi nadhikika; naona dhiki imeniatili imeniumiza; imeniathiri daqiqi kinyunya wabillahi taufiqi na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu zibaqi shaba kheli farasi baghala nyumbu ghurubi magharibi takilahiqi nitakipokea; nitakikaribisha amiqi shimo balaghamu mate mazito yanayotoka kooni ...

Share