In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 97 namli na baraghuthi (wadudu) chungu na mbu shibaye shibe yake athathi vitu Akhuwa tawaeleza, mukhtaswari hadithi Sikuweza kunyamaza, lazima kuihadithi Moyoni yaniunguza, sina wa kustaghithi Innamaa ashkuw bath-thiy wa huzni ila-Llahi Ilahi nastajiri, aghithniy yaa Ghiyathi Ndiwe alimu khabiri, Khaliqu kulla huduthi Ni wewe pweke Mujiri, wa dhukuri na inathi Innamaa ashkuw bath-thiy wa huzni ila-Llahi Rahmani wa jamii, hata na mimi khabithi Aswi nisiyekutwii, hula nikitaabathi Adu’uka yaa Samii, unizidishe mirathi Innamaa ashkuw bath-thiy wa huzni ila-Llahi Nasubiri mja wako, qadi twala talabuthi Naomba faraji kwako, laalla ukabuuthi Na hayano matamko, nasema kwa stighathi Innamaa ashkuw bath-thiy wa huzni ila-Llahi Tammati urahamuye, namli na baraghuthi Kulla mmoja shibaye, kwa kiyasi cha khawathi Ilahi nizidishiye, bustwani na athathi Innamaa ashkuw bath-thiy wa huzni ila-Llahi ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ DUNIYA HAIKO TENA! Msamiati Alfatiha! hili ni tamko linalosemwa na Waislamu wanapoambiwa wasome Sura Al– Fatiha (yaani “Alhamdu”), aghlabu kabla au baada ya kuombwa du’a imekhatimu imefika mwisho qadi madhwaa yamepita; yamekwisha muuminina waislamu naswara wakristo 98 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani yametabadali yamebadilika mubtadaa mwanzo mursali mitume Tumwa Mukhtari Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katawafu amekufa ‘Bubakari Sayyidna Abubakar; Khalifa wa Kwanza wa Waislamu, aliyeshika uongozi wa umma wa Waislamu (632 – 634) baada ya kufariki Mtume Muhammad katika mwaka 632 Umari Sayyidna ‘Umar ibn Khatwaab; Khalifa wa Pili wa Waislamu (634 – 644) Uthmani Sayyidna ‘Uthman bin ‘Affaan; Khalifa wa Tatu wa Waislamu (644 – 656) Alimu hapa amekusudiwa Sayyidna ‘Ali bin Abii Twaalib; Khalifa wa Nne wa Waislamu (656 – 661) idili uadilifu; haki buldani miji iliyoumu iliyoenea dhili tesa umnaqimu khasimu umuangamize adui Fasiri zakalibiwa Tafsiri za Qur’ani zinapotolewa dhuu fatwini watu mahodari ajawidi wasomaji Qur’ani kwa tajwidi maquyudi watu walioshikamana na ibada lizamu adhabu ya kifungo wanaghibishwa baidi wanapotezwa, wanatokomezwa mbali ghanamu kondoo hirimu vijana jahara bila ya kificho; wazi wazi mahashumu waheshimiwa laimu mtu mwenye vitendo viovu ahali huauniwa jamaa husaidiwa madhlumu aliyedhulumiwa darahimu pesa maathamu madhambi Hambo mji wa Hamburg, ulioko kaskazini ya Ujerumani Rumu Roma wamestaqari wametulia mahali [18.118.145.114] Project MUSE (2024-04-24 12:38 GMT) Sarahani 99 bahaaimu wanyama; watu wapumbavu maliki dhwirghamu mfalme mkali kutanaamu kuneemeka angetunaqimu angetuletea nakama; angetuangamiza angezibadhiri angezifuja; angeziangamiza Saidumu mji wa Sodom, ulioangamizwa kwa sababu ya wakaazi wake kupenda liwati, yaani kitendo cha watu wa jinsia moja kulalana Alfatiha! Ammiyna, duniya imekhatimu Hakuna thamma hakuna, bakiya hamu na ghamu Wajinga wasioona, tawambiya kwa nudhumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Duniya haiko tena, akhuwa mkifahamu Huwaje muuminina, Naswara kuwahukumu? Mujuwe kama hakuna, wanakwisha Isilamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Mambo yametabadali, wa duniya ukadimu Zamani yatoka mbali, mubtadaa wa Adamu Hata wote mursali, zimekwisha zao zamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Mwisho Tumwa Mukhtari, katawafu hakudumu Na mwinziwe ‘Bubakari, naye hakustakimu Na maulana Umari, Uthmani na Alimu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Wako wapi Abbasiyya, na hao bin Imamu Idili imepoteya, Madina na Qalzumu Buldani zote piya, na bara ya Maryamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Hii ni mwisho zamani, hao walipoadimu Imeondoka imani, hata leo kwa ayamu Mkitaraji Qarini, mwandikiye makhadimu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Adimu wanao dini, waswalio na swaumu Hawajuwi masikini, dhaifu kuwakirimu Ila wizi na kuzini, na riba iliyoumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! 100 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Na hao wanaoswali, huomba Rabbi Rahimu Rabbi twondolee dhili, umnaqimu khasimu Dua hazitakabali, ni adha kuu yaumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Yatosha mnayosuwa, lenu lipate kutimu Fasiri zakalibiwa, kwa lisani na kalamu Wenye akili hujuwa, hubaki kutayamamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Mashekhe dhuu fatwini, wadurusuo ilimu Ndio walio vitini, wamuamini dhalimu Wahukumiya kanuni, matumbo tele haramu! Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Wako wapi ajawidi, mashekhe li-akramu Kemkemu maquyudi, wamepasiwa lizamu Wanaghibishwa baidi, wachungwa kama ghanamu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Inaondoka sitara, watazameni hirimu! Hutoka hivi jahara, kama wanao wazimu Wanahozi wanyapara, leo ndio mahashumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena Hakuna mtu mwanawe, awezaye mlaumu Mwanangu tunza utuwe, sikae kama laimu Takujazi uchukiwe, ufike kwa mahakimu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Ahali huauniwa, wakakutaka qiyamu Mume akalazimiwa, mambo yaliyo magumu Hana atafasikhiwa, na hayo ni maalumu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Fakiri hahukumiwi, japo kuwa madhulumu Wala baruwa hapewi, japo kwenda na madamu Mwalimu halaumiwi, atowapo darahimu Qadi-madhwaa salamu, duniya haiko tena! Mambasa na Zinjibari, imezidi maathamu Hushinda zote bandari, Ulaya, Hambo na Rumu Wengi wamestaqari...

Share