In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 93 LIZAMU NA DARIZENI Msamiati nusura (kwa) bahati amenusurika lizamu kifungo gerezani darizeni adhabu ya kupigwa viboko kumi na mbili alitiwa mkononi alikamatwa aswahi kweli kabisa penuni vichochoroni twaghi majivuno; kiburi mdongeya kofia ya Kiswahili isiyokuwa na vito na iliyoshonwa kwa cherehani qabihi (mtu) mwovu shaibu mzee ubazazi werevu wa kufanya vitimbi au vioja atayaqani anayakinisha; anapata hakika; anajua taazura izara; aibu kun–ashaddi jiweke tayari Basha Ali93 mwambiyeni, sasa ni kutulizana Zimegeuka zamani, ukamange hapo jana Juzi mzambarauni, fundi alipatikana! Nusura angaliona, lizamu na darizeni! Lizamu na darizeni, hiyo ni khabari kana Zingemwingiya mwilini, adabu ya kufanana Hila na zake fununi, hata asingelipona Nusura angaliona, lizamu na darizeni! Alitiwa mkononi, hiyo aswahi si dhana Akitambaa penuni, Mnyasa wakapambana Akapelekewa pwani, msikiri japo kana Nusura angaliona, lizamu na darizeni ! Ulimughuri urefu, kwa twaghi na kujivuna Miguu isiyo chafu, kama jini Maimuna Na kama si Bin Sefu, kwa Kepteni94 kunena Nusura angaliona, lizamu na darizeni ! 93 Jina mojawapo la Kamange alilokuwa akiitwa na washairi wenziwe. 94 Cheo cha afisa wa wakati wa utawala wa kikoloni, aliyekuwa mkuu wa eneo la Pemba. 94 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kusema naona haya, lakini twataniyana Hakuzidi mdongeya, kanzu alikuwa hana! Watu wakimzomeya, huku wakioneshana Nusura angaliona, lizamu na darizeni ! Kila linalomswibu, yastahiki maana Jitu qabihi shaibu, kukaa kama jununa Halijui ya aibu, domo refu kama ngwena Nusura angaliona, lizamu na darizeni ! Kazi yake ubazazi, kutwa kulala mchana Hanasibiki na kazi, kulima wala kushona Hasafiri hachuuzi, daima: Salamu mwana! Nusura angaliona, lizamu na darizeni Amri ya Kepteni, kila siku aiguna Asema hapatikani, atisha kwa puwa pana Sasa anatayaqani, ya juzi hayako tena Nusura angaliona, lizamu na darizeni! Ukome kwenda usiku, umekupiga mdhana Pemba yote yakushuku, baadhi wakunong’ona Yakuswibu kila siku, taazura na laana Nusura angaliona, lizamu na darizeni! Kaditama asikari, nasikiya wakinena Kamange twamvinjari, shati takwenda kwa Bwana Kun-ashaddi hadhari, utalima na watwana Nusura angaliona, lizamu na darizeni! ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ LAA-YUHIBBU MAN-KAANA…95 Msamiati mtakabari mtu mwenye kiburi; mwenye majivuno sikukubeuwa sikukudharau haijuzu haifai; si sawa kuwatefuwa kuwadharau wanazuoni wa jana wanazuoni wa zamani; wanazuoni waliopita 95 Hiki ni kipande cha mwisho cha Aya ya 36 ya Sura ya 4 ya Qur’ani, chenye maana ya “Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi, wanaojifakhiri” (wanaojisifu). ...

Share