In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

80 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Wa-bihaki Mursali, Ilahi umtaqimu Mja’liye isqamu, utakabali amina ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NAKULAUMU Msamiati ujudi (jambo) lililoko, lipatikanalo au lijulikanalo kuanisi kustarehe ramsa furaha muwadi mpenzi takuapiya yamini nitakuapia; nitakulia kiapo; nitakulia yamini wataakhari wachelewa Bi Kuwini, Sultwana wa Ngereza Bibi “Queen”, malkia wa Uingereza Ewe shada-l-muluki, moyoni waniunguza Nadhani hino ni chuki, aula sikupendeza Madhali kama hutaki, wajibu kunieleza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Ndipo nikakulaumu, maana wewe muweza Akali hata salamu, kijakazi kutumiza Kuondowa malaumu, huzuni kunipunguza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Lipi linaloharibu, kuja tukazungumza? Kama wakhofu taabu, kufika mimi naweza Ni ujudi Waarabu, kuanisi na kucheza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Ramsa hudhuru nini? na hayo si muujiza Wahadhari kitu gani? muwadi nakuuliza Takuapiya yamini, iwapo tayaeneza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Muhali umekwandama, hivi ungajipumbaza La mwisho hata khadima, mtu hutaki agiza Si vyema thama si vyema, sifanye nakukataza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Sarahani 81 Wa kemkem nadhiri, nakuekeya aziza Na wewe wataakhari, kiyasi kuniumiza Lipi unalofikiri, na lisemwalo husoza! Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Tamma wapita njiyani, nisiweze kuuliza Mekufanya Bi-Kuwini, Sultwana wa Ngereza Taji lililo kichwani, na macho ukirembeza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ MUWONGO WA UWONGONI84 Msamiati hashaki tamko lisemwalo kabla ya kumwambia mtu maneno ya matusi; hashakum! mjoli mjakazi arifu mjuzi maamuma neno hili lahusiana na swala katika Uislamu. Na maana yake ni: mtu anayeswali nyuma ya anayeswalisha, au kuongoza swala, yaani nyuma ya imamu. Lakini katika ubeti huu limetumika kwa maana yake ya ziada katika lugha ya kawaida ya Kiswahili. Nayo ni: mtu asiyekuwa na ujuzi au elimu ya kutosha ya jambo fulani, bali hufuata mawazo ya watu wengine zaidani zaidi isma’a majinuni sikiliza ewe mwendawazimu imewakifu imewatosha; imewaridhisha ismuhu jina lake pashao hamu kubwa; pashau auni msaada kafa nyote 84 Kwa mujibu wa mwanawe Sarahani, Bwana Matwar, sababu ya Sarahani kulitunga shairi hili ni kwamba alifikiwa na mtu aliyejiita “Sharifu”. Mtu huyu alikuwa akijidai kwamba ni sharifu, na hali ya kwamba si kweli. Hakuwa Mwarabu wala hakuwa na damu ya Wapemba, bali Sarahani akimjua kwamba ni Mkuyu, kabila mojawapo la makabila ya Kwale, Kenya. Pia alijidai kwamba yeye ni mwanachuoni, na hilo halikuwa kweli pia. ...

Share