In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

78 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Shaba ni kwa muharuma, “Twachuma Hivi” hapandi Hachinji tukale chama, wala machungani hendi Yu Hurumzi daima, katu pengine hashindi Nini kufanyiwa shindi, hata tambi kuvaliwa? Tamati Shaba hawazi, uchafu wote hakondi Angekuwa kama uzi, ila hadhii hawandi Hudhani jumba la kozi, lafunikiza kibundi! Nini kufanyiwa shindi, hata tambi kuvaliwa? MJA’LIYE ISQAMU Msamiati isqamu maradhi Allahumma staani, bismikal adhwimu Ewe Mwenyezi Mungu naomba msaada kwa jina lako tukufu naduuka ya–Manani nakuomba Wewe (Mwenyezi Mungu) iwe kun–fayakuni (niombalo) liwe pasi na kuchelewa; iwe ni (Mwenyezi Mungu) kuliambia “Kuwa!” na likawa ka baraswi na judhamu kama mbalanga na ukoma irufai fil–hali (dua) ipae/ifike juu haraka sihamu chembe cha mshale; kigumba zaqumu mbiliwili; mbigili idhwamu m(i)fupa uzebe upumbavu kwa shuhuri na ayamu kwa miezi na miaka asisikiye kalamu asisikie maneno; awe kiziwi na sururu la-yadumu! – asipate furaha ya kudumu abtali (mtu) aliyeharibikiwa na hali madhumumu anayetajika kwa ubaya umtaqimu umwangamize Allahumma staani, bi-ismikal adhwimu Naduuka ya-Mannani, niamuwe na khasimu Iwe kun-fayakuni, haya nnayonudhumu Mja’liye isqamu, utakabali amina Naimukhuni duniya, wemawe wamukhasimu Iwe ni kumkimbiya, ka baraswi na judhamu Sarahani 79 Pasiwe wa kumwendeya, mtu wa kumrehemu Mja’liye isqamu, utakabali amina Wa-bihaki Jibrili, duwa yangu naitimu Irufai fil-hali, ishuke kama sihamu Jamii ya maakuli, alacho kiwe ni sumu Mja’liye isqamu, utakabali amina Ilahi nihukumiya, ni wewe pweke hakimu Mjuzi wa zote niya, ajili ni madhulumu Madamu amenambiya, takula kama zaqumu Mja’liye isqamu, utakabali amina Rabbi mpe subiyani, amle nyama na damu Amuingiye mwilini, amvugute idhwamu Hali yumo duniyani, halafu hana fahamu Mja’liye isqamu, utakabali amina Ilahi mpe uzebe, ajaye tumbo na pumu Aviringe kama kobe, kwa shuhuri na ayamu Japo kula asishibe, iwe nari jahanamu Mja’liye isqamu, utakabali amina Ya-Rabbi mpe uziwi, asisikiye kalamu Na macho kizuwizuwi, ale uchungu na tamu Kusema awe hajuwi, bi-haki Ibrahimu Mja’liye isqamu, utakabali amina Wana lana wajakazi, jamii binti haramu Sijapo ukamuezi, kwa hiba na kugharimu Mwishowe atakujazi, kheri kufuga bahimu Mja’liye isqamu, utakabali amina Na aliyekuwa wote, vita wakinihujumu Mamaye awe kiwete, asiweze muhudumu Hapa na hapa asote, waleteyane salamu Mja’liye isqamu, utakabali amina Atakayo asipate, tamaa na udhalimu Ili kupata chochote, apate hamu na ghamu Na sasa ngoja ajute, na sururu la-yadumu! Mja’liye isqamu, utakabali amina Kaditama abtali, jinsi yake madhumu Nione kwa siku mbili, umbashiri wazimu [3.16.83.150] Project MUSE (2024-04-19 23:05 GMT) 80 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Wa-bihaki Mursali, Ilahi umtaqimu Mja’liye isqamu, utakabali amina ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NAKULAUMU Msamiati ujudi (jambo) lililoko, lipatikanalo au lijulikanalo kuanisi kustarehe ramsa furaha muwadi mpenzi takuapiya yamini nitakuapia; nitakulia kiapo; nitakulia yamini wataakhari wachelewa Bi Kuwini, Sultwana wa Ngereza Bibi “Queen”, malkia wa Uingereza Ewe shada-l-muluki, moyoni waniunguza Nadhani hino ni chuki, aula sikupendeza Madhali kama hutaki, wajibu kunieleza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Ndipo nikakulaumu, maana wewe muweza Akali hata salamu, kijakazi kutumiza Kuondowa malaumu, huzuni kunipunguza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Lipi linaloharibu, kuja tukazungumza? Kama wakhofu taabu, kufika mimi naweza Ni ujudi Waarabu, kuanisi na kucheza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Ramsa hudhuru nini? na hayo si muujiza Wahadhari kitu gani? muwadi nakuuliza Takuapiya yamini, iwapo tayaeneza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu Muhali umekwandama, hivi ungajipumbaza La mwisho hata khadima, mtu hutaki agiza Si vyema thama si vyema, sifanye nakukataza Vibaya umefanyiza, ndipo nikakulaumu ...

Share