In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Sarahani 75 Lam-Alif; Yee Lam-Alif; Yee, ni mwisho natiya tamma Na fatiha ninuwiye, yaumu wal-ayyaama Amina munitikiye, Rabbanaa thamma wa thamma Rabbi ondowa nakama, wajao tu mashakani ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ITIFAKI NI AULA Msamiati itifaki makubaliano; masikilizano aula bora; afadhali unadhifu usafi ukabaila hali ya kutokana na kabila linaloaminiwa kuwa ni bora hukhuniwa huachwa; huhuniwa ghila pato; kipato si shani si ajabu khiyari mtu au watu walio “bora” wanatiwa qila hawana ithibati; hawaaminiki tujari matajiri ikibala makubaliano hujiri hutokea tula (mtu) mrefu dalila dalili; ishara batwila batili akila akali; chache mno majnuna majnuni; mwendawazimu andhala wanyonge lubu-li-babu kindakindaki wasio tuwa wasio na kasoro au ila dhaifu huwa ni ‘ala (watu) dhaifu huwa watukufu watumiwa sharbela watumiwa ovyo 76 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kupendwa si unadhifu, wala si ukabaila Hupendwa japo mchafu, na jamii zote ila Hukhuniwa maarufu, mwenye mashamba na ghila Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Wala si shani uzuri, kuwa na sura jamala Si asili si fakhari, wala si pambo na kula Wanakhuniwa khiyari, nao wanatiwa qila Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Hukataliwa tujari, wanao mambo fadhila Akapendeza fakiri, ikatosha ikibala Dawamu hayo hujiri, mfupi hushinda tula Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Khafifu huwa mzito, yelekeapo jaala Si samadari na mito, si nadhifu pa kulala Wala hufuwati pato, matumizi na chakula Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Na mimi singalisema, naona tele dalila Kulla nikiutazama, moyo hufuwata mila Ujapo na sura njema, haitoshi ni batwila Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Wangapi nimewaona, werevu wenye akila Vijana vya kiungwana, vyenye siyasa na hila Hali zao majnuna, kwa kupenda andhala Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Wangapi lubu-li-babu, wanao hadhi na dola Vijana wa Kiarabu, wasio tuwa mahala Mapenzi yamewaswibu, dhaifu huwa ni ‘ala Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Kemkemu mabanati, lubu katika kabila Zinawakosa bahati, watumiwa sharbela Kusema sana sipati, Subhana wa-Taala Itifaki ni aula, wala si shani uzuri Kaditama itifaki, aidha na ikibala Bahati ikiwafiki, mapenzi huja ghafula Wangapi wameghariki, mahaba yana madhila! Itifaki ni aula, wala si shani uzuri ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ...

Share