In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

64 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani SARAHANI BIN MATWAR (1841 – 1926) Sarahani bin Matwar alizaliwa Pondeyani, Pemba, kwenye mitaa ya Chake Chake, katika mwaka 1841 A.D. Baba yake akiitwa Matwar bin Sarahan bin Muhammad bin Masoud bin Nasir Al-Hudhury, Hinawy. Babu yake Sarahani alitokea Oman, mji wa Al-Hoqeeni.Yasemekana kuwa babake Sarahani alizaliwa Mombasa katika mtaa wa Kuze, akaoa hapo hapo Mombasa na baadaye akahamia Pemba. Habari hii ya babake Sarahani kuishi na kuoa Mombasa haikupatikana kwa ukamilifu, isipokuwa ya kwamba Sarahani mwenyewe alikuwa akenda Mombasa kuwazuru jamaa zake. Kwa mujibu wa habari zilizopokewa mwaka 1976 kutoka kwa Matwar bin Sarahani, mwanawe Sarahani aliyezaliwa 1910, ni kuwa Sarahani alipotimia umri wa mwaka mmoja, babake alikufa akiwa ni mzee. Wakati huo, Pemba ilikuwa chini ya mfalme wa Unguja, Sayyid Said bin Sultwan. MamayakeSarahaniakiitwaBiAtiyebintiJadibinNasirRuqeishy.Yeyealizaliwa Pemba, akaolewa na babake Sarahani, na akawazaa Sarahani na nduguze, Masudi na Mariyamu (Mwanayamu). Sarahani alikuwa ni kitindamimba. Mwalimu wa kwanza wa Sarahani alikuwa ni mamake, ambaye alisifika kwa elimu na heshima. Miongoni mwa sifa zake ni kuwa alisomeshwa vizuri hata akaihifadhi Qur’ani yote kwa moyo. Wakati huo ilikuwa ni fahari kwa wazazi kuwasomesha watoto wao na kuwahifadhisha Qur’ani. Kwa msingi huu aliokuwa nao, Bi Atiye aliutekeleza wajibu wake wa kuwasomesha watoto wake, kama alivyosomeshwa yeye, na kuwalea kwa malezi mema. Kwa hivyo, mbali na kumsomesha yeye mwenyewe - na kama ilivyo kawaida ya watoto wa Kiislamu - alimtia chuoni kuendelea kujifunza Qur’ani. Bi Atiye hakuridhika mpaka mwanawe alipoihifadhi Qur’ani kama alivyohifadhishwa yeye. Baadaye akampeleka kwa mashekhe kujifunza lugha ya Kiarabu na fani mbalimbali za dini ya Uislamu. Ingawa kwa kizazi Sarahani alikuwa ni mfuasi wa madhehebu ya Ibadhi, mashekhe wa kwanza aliosoma kwao walikuwa ni Sunni. Yaonesha mashekhe wake hawa walimuathiri kwa kiasi fulani, kwani katika ujana wake alifuata madhehebu ya Sunni, na alirejea katika Uibadhi utuuzimani. Miongoni mwa mashekhe waliomsomesha Sarahani ni Sheikh Abdalla bin Amur Al-Azriy. Sheikh huyu alikuja Unguja kutoka Oman. Na Wamazrui wakamleta Pemba ili kuwasomeshea watoto wao; na watoto wengine nao wakanufaika naye. Wakati huo Sarahani alikuwa ashakuwa barobaro. Baadaye Sarahani akenda Unguja ili kusoma kwa mashekhe waliokuwa wakisomeshafanimbalimbalikatikamisikiti.HukoakasomeaTafsiriyaQur’ani, Sharia ya Kiislamu, Fiqhi (ya Sunni na ya Ibadhi) – na fani zihusianazo na Fiqhi, kwa mfano Tarekhe (Historia), Aadab (Fasihi); pia akajifunza Urudhi (Kaida Sarahani 65 za Ushairi) na Qawafi. Katika utuuzima wake, Sarahani alihesabiwa kuwa ni mwanachuoni na alikuwa akiwasomesha fani hizo watu wengine - msikitini na nyumbani kwake. Wakati huo alipokuwa Unguja akisoma, Sarahani alikuwa akirudi Pemba mara kwa mara kuwazuru jamaa zake. Baada ya Sarahani kupata elimu kwa mashekhe wa Unguja, alianza safari za kufanya biashara na kuwazuru wanazuoni (mashekhe) maarufu wa siku hizo katika miji mbalimbali ya Pwani ya Afrika ya Mashariki, na ambao alikuwa akisoma kutoka kwao. Kwa mfano, alikuwa Sarahani akenda Tanga kumzuru Sheikh Hemed bin Abdalla Al-Buhry (babu yake aliyekuwa Mufti wa Tanzania, Sheikh Hemed bin Juma). Sheikh Hemed bin Abdalla alikuwa mwanachuoni maarufu na pia mshairi. Mbali na tungo zake zilizochapishwa vitabu, kuna nyengine ambazo hazijachapishwa. Miongoni mwa hizo ni zile tungo alizokuwa akiimbana na Sheikh Muhammad bin Mshihiri, wa Wasini, kusini mwa Pwani ya Kenya. Huko Tanga Sarahani pia alikuwa akihudhuria darasa ya Sheikh Umar Stambuli, ambaye alikuwa Kadhi wa mji huo wakati huo. Urafiki baina ya Sarahani na Sheikh Hemed bin Abdalla ulishika nguvu na kuendelea mpaka mwisho wa maisha yao. Kwa Sheikh Hemed bin Abdalla, Sarahani pia alijifunza elimu ya Twiba Asili72 , ambayobaadayealiendeleakuisomakutokakwamashekhewakwao.Kadhalika kutoka kwake alijifunza elimu ya Falaki, au Unajimu. Pia akajiendeleza zaidi katika elimu ya Fasihi ya Kiarabu, pamoja na Tarekhe ya Fasihi na ya watungaji wa kale wa Kiarabu, na pia akaisoma Tarekhe ya Kiislamu. Sarahani alivutiwa sana na mashairi ya Kiarabu yaliyotungwa Makka kabla ya Uislamu, na yaliyokuwa yakitongolewa na washairi wenyewe waliokuwa wakishindana. Kwa kuwa Sarahani alikuwa na hifdhi kali, bongo lake liliweza kuyahifadhi na kuyaimba kwa moyo mashairi hayo. Sarahani alikuwa na ndugu wa kike Mombasa, aliyezaliwa na mke wa babake aliyemuoa alipokuwa akikaa Mombasa. Mama yake huyu ndugu yake akiitwa Mwana Isha, ambaye baadaye aliolewa na Bwana Ahmad, na akamzaa Sheikh Said bin Ahmad, ambaye alikuja kuwa Kadhi wa Takaungu na Vanga, miji iliyoko Kenya. Alipokuwa Mombasa kumzuru huyu nduguye wa kike, Sarahani alikuwa akihudhuria darasa za mashekhe wakubwa wa Mombasa, haswa darasa ya Sheikh-ul-Islam, Mwenye Abudi (1844-1922)73 , na Sheikh Suleiman bin Ali Mazrui (aliyekufa 1931)74 . Katika darasa hizi alisuhubiana na Sayyid Twahir bin Abubakar, ambaye alikuwa ni mshika makamu ya Sheikh Suleiman bin 72 Twiba Asili...

Share