-
Kamange Kenda Kaputi
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
58 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani KAMANGE KENDA KAPUTI: (Hamadi bin Khatoro Al-Mazruiy) Msamiati Inna lillahi wa–inna ilayhi raajiuwn, ni sehemu ya tamko, ambalo Waislamu wanalisema wanapofikwa na msiba wa kufiliwa au wanapopashwa habari kwamba mtu fulani amefariki. Maana yake ni: Sisi (sote) twatoka kwa Mwenyezi Mungu, na Kwake tutarejea. ughaiba ughaibu; Akhera mkimuaili mkimlaumu; mkimtuhumu mvunja buyuti mvunja nyumba. Hapa maana ya neno “nyumba” ni ndoa baswiri mwenye busara; mtu anayeona mbele kayaya amemalizika e mrembo alikuwa mrembo kibuhuti mshtuko nikiwahani nikiwapa pole kwa kufikwa na msiba wa kufiliwa iwane ipigane Inna-lillahi mswiba, nawaarifu umati Basha kenda ughaiba, yamemkumba mauti Umefika mkataba, kaja Hadimu Ladhati67 Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Masikini Basha Ali, yuko wapi maimuti! Mlo mkimuaili, kama mvunja buyuti Sasa ametanakali, nazondoke tafauti Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Katwondokeya baswiri, mrembo mtanashati Kalamu-l-makadiri, mtu mwakawe hapiti Duniya kaihajiri, kayaya kama baruti Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Basha Ali e mrembo, pamoja na kharubati Meswifika kulla jimbo, aina kwa ainati Kufa amewacha mambo, kiliyo na kibuhuti Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali 67 Malaika Izraili, ambaye kazi yake ni kutoa roho za binadamu. Kamange 59 Kahajiri makaoye, kahepa uhasharati Dum huko ahamiye, yu sabaa samawati Roho yake ituliye, asiwe na harakati Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Basha Ali akivuma, mshindo kama rakiti Ali mwingi wa hikima, kwa suudi na bahati Mwema mno wa kusema, hata katika korti Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Ila Sheikh Sarahani, mwaliya kwa tashtiti Man-alayhaa-faani68 , itabaki yake dhati Daima yake Manani, kiumbe ni haihati Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali Napita nikiwahani, nandike kaditamati Khalifa wake ni nani, akae juu la kiti? Acheze na Sarahani, iwane miti kwa miti Kamange kenda kaputi, masikini Basha Ali ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KADHWA HAINA MGANGA: (Sarahani) Msamiati kadhwa ajali; kifo enyi mnao simazi enyi wenye huzuni si jaizi haifai mkiombowa mkiomboleza kisuwa nguo Rasuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.); Rasuli Muungamu Mwenyezi Mungu kuitabiri kuzingatia aliyekutakadamu aliyetangulia 68 Hii ni sehemu ya Aya ya 26 ya Sura ya 55, ambayo ni miongoni mwa Aya zielezazo matukio ya siku ya Kiama. Aya yenyewe yasema: Kullu man alayhaa faan; yaani: Kila kilichoko juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka). Na Aya ifuatayo yaendelea kueleza, “Na itabaki dhati ya Mola wako (tu Mwenyewe), mwenye utukufu na hishima.” ...