In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 37 Muhibu ita wenzio, Allah! Allah! Paka Shume Kadiri uwajuwao, mukae njama museme Wala pasiwe mkao, nikosapo niazime Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Enyi wanafunzi wangu, mwaniuwa kwa mzeme Kuna baridi na wingu, mwangojeya kuditime ‘Tajaingiya uchungu, gaga lije liwangame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Wanangu nianjieni, nami kwa watu nivume Nendapo mahadharani, kiulizwa muungame Yaenee mitaani, kwa washoni na wajume Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Paka fanyiza juhudi, wenzio uwaandame Nipate kanzu ya Idi, nijione mfalume Afanyaye ukaidi, talmidhi ni ukame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Tamma na hiyo baruwa, wape kyafa waisome Ambaye hataki towa, akajifanya kangame Shati ‘tamlisha kowa, moyoni ampe chame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ RABBI AMENIPA PERA Msamiati hana jora hana mwenzake Jazira kisiwa hudahadara huzunguka kutirira kutia maringo ibura ajabu kisiraji-lilmunira kama taa inayong’aa situra (neno hili limetumika hapa kwa maana ya “beti”) swaghiruhul -kabira udogo wake ni ukubwa qadi jara amepita 38 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Nisifu wangu mrembo, kwa haiba hana jora Mwenye katwaa na umbo, jamii yote jazira Marini tena utambo, ni mzuri khaswa sura Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi57 Rangi yake ya dhahabu, uso wake mduwara Mimi amenighilibu, rohoni anikwangura Namkiri kwa adabu, ajuwavo msayara Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi Ni shani siku ya kuja, akili hudahadara Na sasa sina mmoja! kyafa wote maadhura Jina siwezi mtaja, Yallah naomba sitara Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi Adimu namna yake, Mkokotoni na Mwera Aswahi yu peke yake, Stambuli58 na Baswara59 Haiwi maringo yake, ajuwavo kutirira! Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi Ni yeye sina wa pili, amma yake ni ibura Umshikapo muwili, huruka kama mpira! Khaswa ukimkabili, humuoneya khasara Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi Puwa yake ya upanga, imesimama mnara Ajiliza kwa uchanga, ni shani akirembwera Na macho huleta anga, kisiraji-li-munira Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi Kaditamati shairi, ni sabaati situra Naaswihi kwa uzuri, swaghiruhu-l-kabira Na ambaye ajasiri, na’fahamu qadi-jara Rabbi amenipa pera, tunda jema la Peponi ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ 57 Kuna mapokezi mengine ambayo yana kibwagizo tafauti: ‘Rabbi amenipa pera, kipendo cha roho yangu’. 58 Mji wa Istanbul, ulioko Uturuki. 59 Basra, mji ulioko Iraq. ...

Share