-
Nipatiyeni Mwatime
- Mkuki na Nyota Publishers
- Chapter
- Additional Information
36 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kukutaka msaada, usidhani ni ujinga Hupatikana faida, na uso kujikuunga Naona tuna muwada, kwako naliya uchanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale ‘Tafungafunga mabuwa, kama mfano wa tenga Pa mlango tazibuwa, nizibe kwa makaanga Si haja kujisumbuwa, ulimwengu una chonga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Sendi kuomba Selemu, wala Makuwe na Finga Haihati akramu, hadhi yangu naichunga Sijifungi mahazamu, haomba kama Wamanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Tele michenza msitu, ‘takata si ya kudanga Sitashindana na watu, wendao Simba Uranga Kijibanda pima tatu, mwenyewe ‘taungaunga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Hukuweza kata puwa, wajihi ukauunga Wajizuzuwazuzuwa, juso govi kimalenga Hali yangu waijuwa, siri ya ndani ni kunga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Mosi moja hudhuruni, daima wagingaginga Hunionei huzuni, kunipa mtu kujenga Nifanyeje masikini, fakiri sina muhanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Tamma yatosha lawama, beti nilizozitunga Kariha haiji vema, hiwaza Bwana wa Shanga Karafuu sijavuna, na muda wazidi songa Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NIPATIYENI MWATIME Msamiati mwatime kishali niuliye nitolee Kamange 37 Muhibu ita wenzio, Allah! Allah! Paka Shume Kadiri uwajuwao, mukae njama museme Wala pasiwe mkao, nikosapo niazime Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Enyi wanafunzi wangu, mwaniuwa kwa mzeme Kuna baridi na wingu, mwangojeya kuditime ‘Tajaingiya uchungu, gaga lije liwangame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Wanangu nianjieni, nami kwa watu nivume Nendapo mahadharani, kiulizwa muungame Yaenee mitaani, kwa washoni na wajume Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Paka fanyiza juhudi, wenzio uwaandame Nipate kanzu ya Idi, nijione mfalume Afanyaye ukaidi, talmidhi ni ukame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu Tamma na hiyo baruwa, wape kyafa waisome Ambaye hataki towa, akajifanya kangame Shati ‘tamlisha kowa, moyoni ampe chame Nipatiyeni mwatime, niuliye sikukuu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ RABBI AMENIPA PERA Msamiati hana jora hana mwenzake Jazira kisiwa hudahadara huzunguka kutirira kutia maringo ibura ajabu kisiraji-lilmunira kama taa inayong’aa situra (neno hili limetumika hapa kwa maana ya “beti”) swaghiruhul -kabira udogo wake ni ukubwa qadi jara amepita ...