In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 35 Ni wangapi makhasimu, tuliyokhasimiyana! Roho tukaisalimu, na mimi tukitakana Mpenzi nikikukimu, mbona twafarikiyana? Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Kwani pendo madhulumu, mwana tumezoweyana Wala sina tabasamu, ya kula na kutafuna Najuwa halishi hamu, linalopita hupona Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Sili kitu nikashiba, moyo ukatulizana Nikikukumbuka twiba, huwa maarifa sina Haunitoki mswiba, illa kwa kurudiyana Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Ulimwenguni maneno, hivi hivi hupandana Ikiwa ni msongano, watu huswameheyana Machungu yasiwe mno, mpenzi si kiungwana Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Kaditamati shairi, watu hukhalifiyana Dawamu mambo hujiri, kisha wakaridhiyana Wendekeza khantwiri, wala hamkufanana! Wagombao hupatana, rudiya watwani wako ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ MWENYEWE TAFUNGAFUNGA56 Msamiati makaanga makarara chonga fitina akramu tukufu mahazamu kitambaa kipana anachojitatiza mwanamume tumboni, hasa wakati wa vita ili kujikinga na silaha kama vile kisu, jambia au upanga; masombo ‘takata nitakata wagingaginga wasitasita kariha ulazimishaji 56 Asili ya shairi hili ni kwamba nyumba ya Kamange ilipobomoka, alimwendea mmojawapo wa jamaa zake kumuomba amsaidie kuijenga. Lakini huyo jamaa yake akawa akimdanganyadanganya na kila siku kumtilia tarehe. Ndipo hatimaye Kamange akampelekea shairi hili. 36 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Kukutaka msaada, usidhani ni ujinga Hupatikana faida, na uso kujikuunga Naona tuna muwada, kwako naliya uchanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale ‘Tafungafunga mabuwa, kama mfano wa tenga Pa mlango tazibuwa, nizibe kwa makaanga Si haja kujisumbuwa, ulimwengu una chonga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Sendi kuomba Selemu, wala Makuwe na Finga Haihati akramu, hadhi yangu naichunga Sijifungi mahazamu, haomba kama Wamanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Tele michenza msitu, ‘takata si ya kudanga Sitashindana na watu, wendao Simba Uranga Kijibanda pima tatu, mwenyewe ‘taungaunga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Hukuweza kata puwa, wajihi ukauunga Wajizuzuwazuzuwa, juso govi kimalenga Hali yangu waijuwa, siri ya ndani ni kunga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Mosi moja hudhuruni, daima wagingaginga Hunionei huzuni, kunipa mtu kujenga Nifanyeje masikini, fakiri sina muhanga Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale Tamma yatosha lawama, beti nilizozitunga Kariha haiji vema, hiwaza Bwana wa Shanga Karafuu sijavuna, na muda wazidi songa Mwenyewe ‘tafungafunga, nipate hema nilale ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NIPATIYENI MWATIME Msamiati mwatime kishali niuliye nitolee ...

Share