In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 33 Kamange: Nimekuja stajiri, katika dola aliya Mimi mtu wa bahari, bara haijaneleya Penye dhara na khatari, Kamange najikhofiya Akhi nataka himaya, na zana kwangu mwenyewe Mugheiry: Shairi limewasili, kwangu limefikiliya Nawaza yangu akili, shauri la kutumiya Ni kheri kufuga ghuli, milayo naisikiya Kwa Qasamu niapiya, kuhozi biladi zangu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NYAMBILIZI Msamiati ujuba hali ya mtu kujifanya anajua kila kitu; ujuvi; ujuaji takaburi kiburi; majivuno mli mlikuwa mlitaqidi mliamini; mlishikilia twibu rojo la mchanganyiko wa vitu mbalimbali ambalo hutumiwa na Waswahili kujipaka mwilini lilo hilo hilo mkitauwa mkichagua kaunyaka aina ya kileo Ujuba na takaburi, hilo kwenu lilikuwa Mkifanyiza jeuri, mkichinja na kuuwa Leo ni bei khiyari, hapana cha kununuwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Mli mkija Unguja, kwa baragumu na siwa Kulla mkitaka haja, hukhalisi kwa baruwa Leo hata pesa moja, hapana kuaminiwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Ziwapi jagaranati, mlizo mkikunjuwa Mkilegeza sauti, na vilemba kuchongowa Sasa mwatamani pati, ingawa ya kuvuliwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! 34 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Mlitaqidi nasibu, “Lete!” “Kaweke!” “Chukuwa!” Rehema na Zainabu, hukanda na kusuguwa Leo mwatamani twibu, mwalisaga lilo liwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Yawapi madarizeni, mliyo mkitauwa Kaunyaka na shampeni, mkitwaa kwa Magowa Leo paka yu mekoni, hakuna cha kuepuwa! Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Yale maji ya barafu, mliyo mkifanyiwa Na mikate maarufu, bisikoti na haluwa Leo mwataka harufu, kutiya katika puwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ WAGOMBAO HUPATANA Msamiati ayyuhal muhibbina ewe mpenzi wetu mjuvi mtu anayejua (mambo) sana watwani mji ashaddu fitina fitina kubwa twiba matibabu hukhalifiyana hutafautiana hujiri hutokea wendekeza unadekeza; unatendekeza Ewe mpenzi azizi, ayyuhal muhibbina Mjuvi wa maongezi, aidha kulla namna Wanipita siku hizi, kama usiyeniona! Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Rudiya watwani wako, uje unipe maana Nijuwe la ndani yako, tupate suluhiana Maneno ya vyako vyako, ndiyo ashaddu fitina Wagombao hupatana, rudiya watwani wako Kisirani siyo haja, mpenzi sikiya sana Watu wakiwa pamoja, hawaachi kugombana Lipitalo hulivuja, hungoja lijalo tena Wagombao hupatana, rudiya watwani wako ...

Share