In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

32 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani ATAKUJA WADHIISHA54 Msamiati ameotama ametotama; amechutama atakuja wadhiisha atakuja kuwapa shida; atakuja kuwatia katika matatizo Mugheiry: Kamange ameotama, mkiya arusharusha Enyi walinda mtama, ndugu nawahadharisha Nyama asiye huruma, fanyeni ya kumtisha Atakuja wadhiisha, kuwafujiya vilimo Kamange: Kamange bure navuma, mambo yamenichokesha Sina haja na khasama, kujipunguza maisha Msije mkanifuma, bure mkanidhiisha Najipitishapitisha, kutazama hali zenu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ AKHI NATAKA HIMAYA55 Msamiati stajiri omba msaada aliya tukufu akhi ndugu (yangu) himaya ulinzi haijaneleya sijaielewa milayo mila yako 54 Kwa bahati mbaya, beti zilizopatikana ni hizi mbili tu. Yamkini hili lilikuwa ni shairi la majibizano marefu. Maelezo yaliyopatikana kuhusu shairi hili ni kwamba ilikuwa ni wakati wa jioni, kiza chaanza kuingia. Muhammad bin Khamis (maarufu kwa jina la Mugheiry) alikuwa nyuma ya sebule yake huko Finya, Pemba, akishughulika na kutengeza karafuu. Hatua chache kutoka pale alipokuwako, mara Mugheiry akamwona Kamange yuwenda kwa kunyapanyapa. Mugheiry akashuku kwamba lazima Kamange ana mpango fulani karibu na mtaa huo. Akitahamaki, Kamange akajikuta yu uso kwa uso na swahiba yake, Mugheiry! Hapo hapo Mugheiry akatokwa na ubeti. Yasemekana kwamba Kamange, kutokana na kushtukizwa hivyo, hakuwa na jawabu ya nguvu, kama ilivyokuwa kawaida yake, bali alibaki akilalama tu. (Abdurrahman Saggaf Alawy) 55 “Beti tulizozipata ni hizi mbili tu, ingawa shairi lenyewe lilikuwa refu. Tuliambiwa kwamba mtu aliyekuwa akizijua kwa moyo beti zote za majibizano baina ya washairi hawa wawili ni Sheikh Diwani bin Muhammad Al-Maamiry. Hadithi ya majibizano haya ni kwamba Kamange alikusudia kufanya ziara fupi Wasini, Pwani ya Kenya. Mugheiry akenda kwa Kamange kurakibisha mpango huo.Yasemekana kwamba Mughery hakumkubalia. Siku chache kabla ya safari yake hiyo, Kamange akashikwa na maradhi na akafa baada ya muda mfupi.” (Abdurrahman Saggaf Alawy) Kamange 33 Kamange: Nimekuja stajiri, katika dola aliya Mimi mtu wa bahari, bara haijaneleya Penye dhara na khatari, Kamange najikhofiya Akhi nataka himaya, na zana kwangu mwenyewe Mugheiry: Shairi limewasili, kwangu limefikiliya Nawaza yangu akili, shauri la kutumiya Ni kheri kufuga ghuli, milayo naisikiya Kwa Qasamu niapiya, kuhozi biladi zangu ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ NYAMBILIZI Msamiati ujuba hali ya mtu kujifanya anajua kila kitu; ujuvi; ujuaji takaburi kiburi; majivuno mli mlikuwa mlitaqidi mliamini; mlishikilia twibu rojo la mchanganyiko wa vitu mbalimbali ambalo hutumiwa na Waswahili kujipaka mwilini lilo hilo hilo mkitauwa mkichagua kaunyaka aina ya kileo Ujuba na takaburi, hilo kwenu lilikuwa Mkifanyiza jeuri, mkichinja na kuuwa Leo ni bei khiyari, hapana cha kununuwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Mli mkija Unguja, kwa baragumu na siwa Kulla mkitaka haja, hukhalisi kwa baruwa Leo hata pesa moja, hapana kuaminiwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! Ziwapi jagaranati, mlizo mkikunjuwa Mkilegeza sauti, na vilemba kuchongowa Sasa mwatamani pati, ingawa ya kuvuliwa Hadi ni kufilisiwa, hadi kuuza sahani! ...

Share