In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 31 TWAWAFUMA KWA UBUWA Msamiati kalili chache twejuwa twajua; tukijua vikawaghuri vikawadanganya wakadhabihiwa wakachinjwa Sisi hatuweki miko, maradhi yasiyopowa Ya-Ilahi Mngu yuko, Ya-Rabbi atatuvuwa Huyo mwinyi chokochoko, siri tumeifunuwa Twawafuma kwa ubuwa, ndege wana hila gani? Si kalili majasusi, hikima tulizopewa Ndege hawana kisasi, tangu zamani twejuwa Tutawapiga risasi, mitungo tukichukuwa Twawafuma kwa ubuwa, ndege wana hila gani? Makoo yako nyumbani, ya karibu kuanguwa Tuna tamaa mwishoni, hutataka kuyauwa Na ninga tele mwituni, hivi sasa twasuguwa Twawafuma kwa ubuwa, ndege wana hila gani? Wako hao usufuri, ambao ni waelewa Humwagiwa kumpuri, na vichanga vya haluwa Hudona vikawaghuri, mara wakadhabihiwa! Twawafuma kwa ubuwa, ndege wana hila gani? ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ...

Share