In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 23 Sharafa hilo la nini? Ni la bangi au pombe? Ni afa za Firauni, kumbakumba na majumbe Tahayuri za shetwani, kupiga vyanda na kumbe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Sarahani nakwambiya, ndugu yangu sinigombe Ukhalifa ni udhiya, uhadhari unyambembe Ijaza haijangiya, ndipo ukatwe na nyembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Sarahani u mkinzi, ndipo daima nikwimbe Ridhiya uwanafunzi, ukome usijigambe Kwani hujajuwa kazi, pa mbizi wala mikambe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Tamma mambo na wenyewe, ijaza shati uombe Bure usijisumbuwe, si vyema usijitambe Dudu kome nalambiwe, lisiliye penye pembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ DORIYA KAPATIKANA! Msamiati Rabbi–takabali– minna rabbi tutakabaliye/tukubaliye (dua zetu) lizamu na darizeni adhabu ya kupigwa viboko kumi na mbili madhila mateso mdhana kisirani; ukorofi maghibu upepo mkali mmande upepo Nataka omba Jalali, itikiyani “Amina” Muliyo Ntambwe Nyali, na watu wa Mbilingana Chwaka hadi Tandawili, Tumbe na Wingwi ya Pwana49 Doriya50 kapatikana, naende mbele afike 49 Haya ni majina ya vitongoji mashuhuri vya Pemba. 50 Doriya alikuwa ni askari wa gereza. 24 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani Naende mbele afike, Pemba asirudi tena Jamii wanusurike, yawaondoke mahana Khuduma waitumike, pasiwe kusukumana Doriya kapatikana, naende mbele afike Tulimuona Kungoni51 , alivyo akikazana Kwa bakora mikononi, na watu kuwatukana Lizamu na darizeni, uwongo mnapambana Doriya kapatikana, naende mbele afike Hapakuwa na nafasi, illa akishuka Bwana Aondokapo ni basi, kupumzika hakuna Yalimpita kiyasi, mamboye makubwa sana Doriya kapatikana, naende mbele afike Hapakuwa na julusa, ya tumbaku kuombana Illa kwa kando kabisa, atakaye kutafuna Nusuraye Babu Nywesa, kumshukiya fitina Doriya kapatikana, naende mbele afike Walio wakimwegama, masheha tuliyaona Ni Ramadhani wa Juma, watu waliokutana Na Jadi wa Kidorima, jamii wanyamazana Doriya kapatikana, naende mbele afike Rabbi zidi yamzidi, Allahumma Maulana Iwe saada suudi, Rabbi-takabali-minna Muondowe asirudi, Pemba libakiye jina Doriya kapatikana, naende mbele afike Mola hawachi mjawe, madhila wakasongana Nawaarifu mjuwe, watumwa kwa waungwana Doriya na mchungawe, kafa walibakizana Doriya kapatikana, naende mbele afike Hajuwi Pemba peremba, haufai ujagina? Mashumu yakikukumba, haukutoki mdhana Nenda kamwulize Simba, dola ilivyombana Doriya kapatikana, naende mbele afike 51 Kungoni ni mahali ambapo mahabusu walikuwa wakifanya kazi ya kuilaza milima. [18.117.165.66] Project MUSE (2024-04-19 09:36 GMT) Kamange 25 Niyatili matulubu, twakuomba Subhana Yamvumiye maghibu, kusi na mmande pana Kwa baraka za Habibu, Musa bin Imrana52 Doriya kapatikana, naende mbele afike Tamma ende mwana kwenda, Ilahi ndiwe Rabbana Ende posi ya Uganda, ikamshukiye lana Rabbi haya twayapenda, hima tupate bayana Doriya kapatikana, naende mbele afike ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ KWANI MTOTO KITUMBO...?53 Msamiati mtoto kitumbo mtoto mchanga; mtoto mdogo akhuwa ndugu yangu usungo hali ya kuwa mjinga wa mambo yahusianayo na unyago fyuka shuka tambo mtego ndembo tembo; ndovu asadi simba ndimi ni mimi udil–karaha aina ya udi ambao hutafunwa na mtu mwenye ugonjwa wa baridi yabisi kwa ajili ya matibabu huharikisha hutikisa; hufanya (kitu) kikawa na harakati 52 Nabii Musa bin Imran. Katika ubeti huu, Kamange yuwamuomba Mwenyezi Mungu amgharikishe huyo Doriya, kama alivyomgharikisha Firauni na watu wake walipokataa kumfuata Nabii Musa, baada ya kuwalingana kwamba wafuate mafunzo aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 53 “Nilizipata hizi beti nne za shairi hili katika daftari ya babangu, marehemu Mwinyi Alawy. Mwanzo sikujua kama shairi hili ni la kilma na jawabu mpaka baada ya kujuana na Matwar bin Sarahani. Yeye ndiye aliyenieleza kwamba shairi hili lilikuwa ni jawabu ya Sarahani kumtetea mwanawe, Salim bin Hemed. Huyu Salim bin Hemed alikuwa ni mjukuye Kamange kwa nasaba. Yasemekana kwamba Sarahani alimfunzia Salim ende akamtongoze msichana, ambaye Kamange alikuwa ana wivu naye. Kamange alipojua kwamba Salim amfanyia jeuri ya kumtongozea msichana wake, akapandwa na hasira kubwa, kama lionyeshavyo shairi. Kwa bahati mbaya haikuwezekana kuzipata beti zote za shairi hili; kwa hivyo hili halikukamilika. (Abdurrahman Saggaf Alawy) ...

Share