In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 21 Ndimi Kongwe la Kisiwa, la tangu Abu na tangu Mnyasa hajanijuwa, aja niwaziya pingu Bilashi ajisumbuwa, halichaniki hangungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Ni mwanzo wa idmari, Mnyasa kushika nungu Ashikwe na inkisari, apande juu ya fungu Sirikali imbari, achukize kwa Wazungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Tamma siwezi andika, naona kizunguzungu Mnyasa himkumbuka, natamani pigwa rungu Mangapi aloyataka, ameyadafii Mngu! Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ULIPITA ‘SHI NA YOMBE47 Msamiati nyimbiri aina ya shanga ndogo, nyeupe zipatikanazo baharini unyanje werevu; uhodari kisibu aibu kifukumkunye kwa siri lidumbe liseme penyepenye fununu gube kinyume; hiana mijumbe inadi milayo mila yako warombe makuwadi; magawadi akuzengeya akutafuta 47 “Ulipita ‘shi na yombe”, kwa maana ya ulipita ukingoni mwa dimbwi la maji. Yaani ulisalimika na hatari au madhara; ulinusurika; uliponea chupuchupu. “Kwa mujibu wa alivyonieleza Sheikh Salim bin Aliy AlMundhiry , ni kwamba Kamange alilitunga shairi hili baada ya Sarahani ‘kumwoa siri’ bibi mmoja aitwaye Panza wa huko Gando. Yasemekana usiku mmoja Sarahani alikwenda nyumbani kwa Panza akidhania kwamba hakuna aijuaye siri yake hiyo. Aghlabu, mtu aliyeoa siri hupenda kwenda kwa huyo mke wa siri usiku usiku, ingawa ndoa yenyewe ni ya halali. Hata hivyo, baadhi ya watu waliijua siri hiyo, na wakataka kumkashifu Sarahani. Walivyofanya ni kwamba watu walimvizia Sarahani karibu na nyumba ya huyo mkewe wa siri. Sarahani alipofika mlangoni tu, mara watu watatu waliokuwa wamejibanza mikarafuuni wakajitokeza ili kumdhihirishia Sarahani kwamba wamemwona. Wadhihaki wa Sarahani wasema kwamba Sarahani aliyavua makubadhi yake akayashika mkononi na kuanza kutimka mbio, huku wale watu watatu wakimwandama. Baada ya kisa hicho kutokea, Kamange alimzuru Sarahani, ambapo Sarahani akamsimulia rafikiye, Kamange, mkasa uliomfika.” (Abdurrahman Saggaf Alawy) 22 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani tahayuri hali ya kuona haya (kwa sababu ya kutenda jambo ovu au lisilopendeza) mkinzi mkinzani; mshindani; mkaidi Muhibu neleza vyema, wala usifumbefumbe Ni ada ya mkulima, haachi katwa na jembe Siulizi kwa khasama, sina fila hata chembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje48 Uliuvuka wa Chanje, wengeliwa na wakombe Wengelitungwa kipunje, kama nyimbiri na mbe Wengekwishiya unyanje, nusura wende ukambe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Ushanitiya kisibu, haya yote yako Tumbe Wanifanyiya aibu, Mtambwe hadi Mvimbe Weshapata kisibabu, Majimbutu na Kanambe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Wala usinidanganye, sinifiche hata chembe Wacha kifukumkunye, ulilonalo lidumbe Nasikiya penyepenye, hawana siri viumbe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Kumbe vile Sarahani, kusema zembe uzembe Kwa gube huwezekani, una ngeya kama ng’ombe! Wapenda mitambuuni, wapiga wenziyo vyembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Wanicheka wanizoma, wanitoleya mijumbe Leo jinalo lavuma, tangu Panza umchumbe Kulla mcheka kilema, hafi illa kimkumbe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Wataka vyako pekeyo, vya wenzio uvirambe Khiyana ndiyo milayo, utatimbwa na warombe Akuzengeya chezoyo, Mdahoma akutimbe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje 48 Mto wa Chanje. Huu ni mto ulioko Pemba, karibu na Gando. [18.222.69.152] Project MUSE (2024-04-16 20:55 GMT) Kamange 23 Sharafa hilo la nini? Ni la bangi au pombe? Ni afa za Firauni, kumbakumba na majumbe Tahayuri za shetwani, kupiga vyanda na kumbe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Sarahani nakwambiya, ndugu yangu sinigombe Ukhalifa ni udhiya, uhadhari unyambembe Ijaza haijangiya, ndipo ukatwe na nyembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Sarahani u mkinzi, ndipo daima nikwimbe Ridhiya uwanafunzi, ukome usijigambe Kwani hujajuwa kazi, pa mbizi wala mikambe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje Tamma mambo na wenyewe, ijaza shati uombe Bure usijisumbuwe, si vyema usijitambe Dudu kome nalambiwe, lisiliye penye pembe Ulipita ‘shi na yombe, ukauvuka wa Chanje ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ DORIYA KAPATIKANA! Msamiati Rabbi–takabali– minna rabbi tutakabaliye/tukubaliye (dua zetu) lizamu na darizeni adhabu ya kupigwa viboko kumi na mbili madhila mateso mdhana kisirani; ukorofi maghibu upepo mkali mmande upepo Nataka omba Jalali, itikiyani “Amina” Muliyo Ntambwe Nyali, na watu wa Mbilingana Chwaka hadi Tandawili, Tumbe na Wingwi ya Pwana49 Doriya50 kapatikana, naende mbele afike 49 Haya ni majina ya vitongoji mashuhuri vya Pemba. 50 Doriya alikuwa ni askari wa gereza. ...

Share