In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

Kamange 19 Vyako ndiyo kudanganywa, khaswa zamani za leyo Vyako chako hunyang’anywa, daima ukenda mbiyo Vyako mwishowe husonywa, na wingi wa mazomeyo Vyako hubadili moyo, ukagomba na jirani Vyako hakika si njema, tamati ni kishiliyo Vyako usipoinama, waudhika maishayo Vyako hushikizwa tama, nawe ukasema: Ndiyo Vyako hubadili moyo, ukagomba na jirani ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ MASHUMU YANGU Msamiati amekoroweza ameshindwa na mambo mashumu machungu hichi changu! hili ni tamko ambalo mtu hulitumia kusisitizia onyo analompa mtu. Ni kama kumwambia, “Wewe wafikiri kwamba hili nilisemalo halitakufika, au halitatokea, lakini nakuhakikishia kwamba litakuwa, na litakapokufika utakuja kuyakumbuka niliyokwambia.” dahari miaka mingi pungu mnyama aliyefanana na ng’ombe aihajiri aihame; aigure koma uwezo au nguvu, haswa ziaminiwazo kwamba zatokana na mizimu hakii mtungi hapandi mtungi; hafai fatini mtu mwerevu vitingu vitimbi; vitimvi; hila bilashi bila ya sababu hangungu aina ya kitambaa kinene, ambacho si rahisi kuchanika idmari uvunjifu nungu mnyama mdogo mwenye miba, ambayo hutumiwa kushonea kofia za vito za Kiswahili inkisari kasoro fungu mwamba 20 Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani imbari ijitenge naye ameyadafii ameyakinga; ameyalinda Amekoroweza fundi, mwinyi fingo na mizungu Azamiyaye minandi, bahari ya vunja tungu Hazaini penye lindi, hupita jiza na wingu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa42 yatamwondowa Inshallah yatamwondowa, amepekuwa mvungu43 Posini atamwondowa, si urongo hichi changu! Ni mbugu nasifiwa, enda nivunjiya jungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Akojoleya kilinge, kilichozikiwa nyungu Wacha mwiba umsonge, anywe maji kwa furungu Dahari haishi zinge, ulimwengu ni ukungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Tampigisha kwa buo, gombe pofu; kongwe pungu Aihajiri Takao44 , Kamange kwa koma zangu Juweni hana makao, nilivyomeza machungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Enyi mwendao Ging’ingi, mpandao pasi pingu Jongoo hakii mtungi, Mnyasa hupanda mbingu! Hana kheri Mwiirangi, kwa kula wali na dengu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Anileta kwa Kipeni45 , haujuwi ulimwengu Simba46 yeye ni fatini, ajuwa kula vitingu Kesho Mzambarauni, tahama miko na vyungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa 42 Mnyasa alikuwa ni askari wa Polisi aliyekuwa akichukiwa sana na wakazi wa Pemba kwa sababu ya maonevu aliyokuwa nayo na kwa kuwavunjia heshima watu. Kamange alilitunga shairi hili kumuapiza Mnyasa baada ya kumkamata Kamange alipovunja sheria ya kafyu usiku. Baada ya kukamatwa, Kamange alilazwa korokoroni mpaka alipotolewa kwa amri ya Sheikh Muhammad bin Seif Al-Jeneby, aliyekuwa Naibu wa Kamishna wa Pemba. 43 Mapokezi ya kwanza ya shairi hili yalitokana na Sayyid Hassan bin Nasir (maarufu kwa jina la Mwinyi Alawiy). Halafu likakamilishwa baada ya kupatikana katika nyaraka za Sheikh Salim bin Aliy Al-Mundhiry, aliyekuwa Mudiri wa Wete, Pemba, (na ambaye alifariki dunia katika mwaka 1972 akiwa na umri wa miaka 70). Kwa mujibu wa Sheikh Salim, yeye aliupokea ubeti huu kutoka kwa watu waliokuwa wakiishi na Kamange, hivi: Posini taondolewa, afungwe kamba na mbungu Ni mvungu nasifiwa, nimpaze kama pungu Na hivi adurusiwa, hafisi kila kitingu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa 44 Hili ni jina la mahali Pemba. 45 “Kipeni” ni jina ambalo wenyeji wengi wa Pemba walikuwa wakimwita Captain Tukmen, aliyekuwa Kamishna, Pemba, wakati wa utawala wa ukoloni wa Mwingereza. Mahakama yalikuwa chini yake. 46 Huyu alikuwa ni mmojawapo wa maaskari, ambaye akiaminiwa kwamba alikuwa na fitina nyingi. [3.17.181.21] Project MUSE (2024-04-26 05:52 GMT) Kamange 21 Ndimi Kongwe la Kisiwa, la tangu Abu na tangu Mnyasa hajanijuwa, aja niwaziya pingu Bilashi ajisumbuwa, halichaniki hangungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Ni mwanzo wa idmari, Mnyasa kushika nungu Ashikwe na inkisari, apande juu ya fungu Sirikali imbari, achukize kwa Wazungu Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa Tamma siwezi andika, naona kizunguzungu Mnyasa himkumbuka, natamani pigwa rungu Mangapi aloyataka, ameyadafii Mngu! Inshallah mashumu yangu, Mnyasa yatamwondowa ✳ ✳ ✳ ✳ ✳ ULIPITA ‘SHI NA YOMBE47 Msamiati nyimbiri aina ya shanga ndogo, nyeupe zipatikanazo baharini unyanje werevu; uhodari kisibu aibu kifukumkunye kwa siri lidumbe liseme penyepenye fununu gube kinyume; hiana mijumbe inadi milayo mila yako warombe makuwadi; magawadi akuzengeya akutafuta 47 “Ulipita ‘shi na yombe”, kwa maana ya ulipita ukingoni mwa dimbwi la maji. Yaani ulisalimika na hatari au madhara; ulinusurika; uliponea chupuchupu. “Kwa mujibu wa alivyonieleza Sheikh Salim bin Aliy AlMundhiry , ni kwamba Kamange alilitunga shairi hili baada ya Sarahani ‘kumwoa siri’ bibi mmoja aitwaye Panza wa huko Gando. Yasemekana usiku mmoja Sarahani alikwenda nyumbani kwa Panza akidhania kwamba hakuna aijuaye siri yake hiyo. Aghlabu, mtu aliyeoa siri hupenda kwenda kwa huyo mke wa siri usiku usiku, ingawa ndoa yenyewe ni ya halali. Hata hivyo, baadhi ya watu waliijua siri hiyo, na wakataka kumkashifu Sarahani. Walivyofanya ni kwamba watu walimvizia Sarahani karibu na nyumba ya huyo mkewe wa siri. Sarahani alipofika mlangoni tu, mara watu watatu...

Share