In lieu of an abstract, here is a brief excerpt of the content:

10 WAKAMAGETA Inafahamika kwamba Ramogi alikuwa na watoto wafuatao: 1. Achol, 2. Adhola, 3. Ligwara, 4. Gial, 5. Aluru, 6. Lango na 7. Kitgum. Walianza kutawanyika pole pole, wengine wakitelemka bondeni mwa Mto Nile, na wengine walipitia Ziwa Victoria, wakipiga makambi yao katika visiwa na kutelemka bondeni pole pole. Na wengine walifuata nchi kavu. Kuna jamaa,wenyeasiliyaLuo,ambaowakomipakanimwaKongonaUganda, sehemu inayoelekea Tanganyika. Jina lingine wanalotumia ni Jonam, na wao ndiyo bado inaaminika kwamba wanasema Kijaluo cha asili, wao pamoja na Acholi kidogo, na wanatania makabila mengine ya Wajaluo kwamba wao wanasema lugha ya wanawake, wakimaanisha kwamba wengine wanaoa makabila mengine na mwisho wanachanganya lugha, mwisho lugha yao kiasili inapotea. Hata hivyo Waluo walioko Sudan bado nao wanadai kwamba wao ndiyo Waluo asilia ukiacha wengine walioingia Kenya na kusambaa hadi Tanzania. Mwanzo wa Wakamageta na Kuhama kwao Watu wa Kamageta ni kweli haijulikani kabisa kwamba Mzee Abuya, 10 KAMAGETA It is said that Ramogi had children called, 1. Achol,2. Adhola, 3. Ligwara, 4. Gial, 5. Aluru, 6. Lango, and 7. Kitgum. They began to separate slowly with some coming down along the banks of the river Nile, and others passing slowly down the shores of Lake Victoria, establishing camps on the islands as they went, while others travelled on the mainland. There are some people of Luo descent who are found at the border between Gongo and Uganda, going toward Tanzania. The other name they use is Jonam. It is believed that these people still speak the original Luo language. These people, along with the Acholi people, tease the other Luo groups of speaking the language of women, meaning that the others who marry women from other ethnic groups in the end mix the languages and eventually their original language disappears. Even so, the Luo in the Sudan still claim that they are the original or authentic Luo, excluding those who spread out into Kenya and Tanzania. Kamageta Origins and Migrations It is true that most Kamageta do not know that Mzee Abuya, who is the [18.226.150.175] Project MUSE (2024-04-25 05:43 GMT) 206 SURA YA KUMI ambaye ndiyo asili ya Kamageta wanaokaa hapa Tanganyika, kwamba alikuwa ni mtoto wa Mageta. Ni vigumu sana kuelewa ila inaeleweka kwamba alipokuwa katika Kisiwa cha Mageta siku moja akiloa samaki, upepo mkali ukakata matende (abuoro) ambayo alikuwa amekalia, basi upepo ukampeleka ziwani mbali sana, na akakaa ziwani kwa muda mrefu akiwa anazidi kutega samaki mbichi na kula pamoja na mizizi ya mimea ya ziwani yaliyokuwa yakielea majini. Siku nyingine upepo ulivuma ukielekea nchi kavu ikampeleka uvukoni, mahali alipokuepo mzee moja Lir (Kaler) akivua samaki. Na akamuokota na akampeleka kwake na kumnyoa na alipoulizwa anatoka wapi au kwa nani, alisema kwa Mageta, akionyesha kisiwa hicho ziwani. Tokea hapo alipooa na kuzaa, watoto wake wakaitwa Kamageta. Lakini bado utakuta Kamageta wengine katika sehemu ya Wara Kano, Imbo, Sakwa, Chula na ni mchanganyiko wa wale waliohama kutoka kisiwa cha Mageta na ukoo wa yule aliyookotwa na Mzee Lir, katika mji wa Sakwa. Mageta alikuwa Mzee wa Kamageta, ambaye alitangulia katika Kisiwa cha Mageta na akakipa jina lake. Mzee Lir wao pia walitoka mapema katika Kisiwa cha Mageta, na wengine wengi kama tulivyotaja hapo hawali. Na inajulikana kwamba watu hawa walioko Kenya na Tanzania wao walipita Kisiwa cha Mageta na hapo walishambuliwa sana na maradhi ya Malale na Ndui na wengine wakatelemka bondeni, sehemu ya Sakwa. Neno hili Sakwa ni mchanganyiko ya watu wasioweza kutulia Sakini au Yogini, maana pale kila mtu aliposhuka bondeni alikimbilia kujenga mji wake kando ya ziwa, ili mlango wake uelekee ziwani. Kwa hiyo pilika pilika ile ya kung’ang’ania mahali pazuri, ndiyo sehemu hiyo ikajulikana kuwa ni Sakwa. Ukoo mkubwa, kama vile Karachuonyo, Kanyamwa, Kano na mengine wametokea Sakwa. Na wengine walizungukia nchi kavu kama wale wa Alego, Gem, Ugenya, Kadimo na wengine. Wao walidharau waliopita katika Kisiwa cha Mageta, wakisema hao walikuwa waoga wa kupambana na wanyama wakali kama vile, simba, tembo, chui na mengine pia, kwamba waliogopa kupigana vita na makabila waliokuwa njiani mbele yao.1 Wengine wanaosimulia mwanzo wa Wakamageta wanasema kwamba Mageta mkubwa yeye alikufa katika kisiwa cha Mageta. Mtoto wake aliyeitwa kwa jina lake yeye alivuka na matende na wenzake na wakaja hadi Uyoma pale palikuwepo watu wa Sakwa na baadhi ya makabila mengi. Alikaa pale na siku moja walikosana na ndugu yake Raya. Akakimbilia kandokando ya ziwa akawa analala ndani ya 1 Mzee Opanga, mtoto wa Oole, Oole wa Osoro, Osoro wa Owuor, Owuor wa Randa, Randa wa Madhe, Adhe wa...

Share